Friday, 2 June 2017


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo kwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, kwenye ufunguzi wa semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Gabriel Silayo alisema, semina hiyo inalenga kuwandaa kwa kuwapa mafunzo watumishi wa umma ambao wanatarajiwa kustaafu hivi karibuni, ili hatimaye wastaafu kwa amani.
“Na kwa kufanikisha hilo, tunao maafisa wetu watatoa mada mbalimbali, wapo washirika wetu, SIDO, na mabenki kama vile NMB, CRDB, TPB, MCB na UTT, ambao watatoa elimu ya namna bora ya kutunza na kutumia fedha zako za mafao.” Alibainisha Bw. Silayo.
Bw. Silayo pia alisema, kwa kutambua kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kauli mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi”. “Na ndio maana tumewaleta SIDO hapa ili wawaelimishe jinsi mtakavyoweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo baada ya kustaafu utumishi wa umma na ndugu zangu napenda niwahakikishie hilo linawezekana.” Alisema
Alisema semina hiyo itakuwa ya siku mbili na kwamba, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ataifungua rasmi kesho Jumamosi Juni 2, 2017.
Zaidi ya watumishi 300 kutoka sekta mbalimbali za utumishi wa umma kwenye wilaya zote za mkoa wa  Mwanza wanahudhuria semina hiyo ya mafunzo.
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
 Meneja Pensheni wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, akitoa mada juu ya maandalizi na fursa za wastaafu
 Afisa Mwandamizi wa Utafiti wa PSPF, Bw. Mapesi Maagi, akigawa vitendea kazi kwa washiriki wa semina mwanzoni mwa mafunzo hayo

 Bw. Silayo, (Kushoto), akiteta jambo na Meenja wa Mipango na Utafiti wa PSPF, Bw. Luseshele Njeje.
 Mshiriki akizunguzma wakati wa semina hiyo
 Afisa Uhusino Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa
Mshiriki akinukuu kilichokuwa kikiendelea
 Wanasemina wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa
 Baadhi ya wadau wa PSPF, na washiriki wa semina wakifuatilia mada zilziokuwa zikitolewa
 Washiriki wa semina wakiwa kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo BoT jijini Mwanza
 Bw. Silayo, (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Meneja wa Fedha wa Mfuko huo, Bw.Lihami Masoli
 Kuonyesha semina hiyo ilikuwa muhimu kwa wastaafu hawa watarajiwa, mshiriki wa semina akinakili kwa uangalifu mkubwa yaliyokuwa yakielezwa (mafunzo)
 Afisa Mfawidhi wa PSPF, mkoani Mwanza, Bw.Salim Salum, akifafanua baadhi ya hoja zilizojitokeza. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo na katikati ni Meenja wa Pensheni wa Mfuko huo, Bw. Mohammed Salim
 Sehemu ya washiriki wa semina
 Mshiriki akipitia ratiba
Washiriki hawa wakipitia vipeperushi vya PSPF vyenye taarifa mbalimbali za Mfuko
Reactions:

0 comments:

Post a Comment