Friday, 16 June 2017

2
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akiwa kwenye mazungumzo na Mhandisi Uendeshaji na Matengenezo, Yinus Krick kutoka Kampuni ya Lahmeyer na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi naUsafi wa Mazingira (LUWASA), Mhandisi, Riziki Chambuso (katikati).
1
Katibu Mkuu Wizara ya Maji naUmwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akipata maelekezo kuhusu ramani ya ujenzi wa mradi wa Ng’apa kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa Mradi, Innocent Mgaya
unnamedMoja ya miundo mbinu  inayojengwa kwenye mradi  wa maji wa Ng’apa, mjini Lindi.
3
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya miundo mbinu inayojengwa kwenye mradi wa maji wa Ng’apa, mjini Lindi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (LUWASA), Mhandisi, Riziki Chambuso
NA MWANDISHI WETU, LINDI
KATIBU Mkuu waWizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Ng’apa mkoani Lindi.

Prof.Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi huo ambao mapema mwaka huu ulimkasirishavibaya Rais John Magufuli na kufikia hatua ya kjuzuia hati za kusafiria za wakandarasi wa kampuni ya India iliyopewa kazi ya kukamilisha mradi huo.

Mradi huo mkubwa, ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Lindi (LUWASA)

“Hali ya huduma ya maji Lindi si nzuri, ukizingatia huduma ya maji kwa sasa inakidhi asilimia 40 tu ya mahitaji ya wakazi wa mji huu, kwa mradi huu wa Ng’apa ukikamilika utatoa huduma ya maji kwa asilimia 100 kwa wakazi wa mji wa Lindi, alisema Prof. Mkumbo.
“Nimefika hapa kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais juu ya mradi huu, na kwa hali ilivyo, mmenifurasha sana kwani maendeleo ya utekelezaji wa mradi ni ya kuridhisha sana.” Alisema Profesa Mkumbo.
Hata hivyo haijaelezwa mradi huo unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 29, utakamilika lini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment