Monday, 5 June 2017

Mgeni rasmi katika shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano Vita dhidi ya Ukiwmwi, Dkt. Tulia Ackson akiwa na Kaimu Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za kulevya, Dkt. Faustine Ndugulile wakiimba na kupiga makofi, muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi hilo ambalo limeratibiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine, (GGM).

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro,lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson kizungumza wakati wa kutoa baraka kwa wanaharakati 89 wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya GGM, na Acacia wanaoshiriki zoezi panda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano, dhidi ya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Baadhi ya viongozi wa wilaya za Hai na Moshi mjini wakifuatalia  shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa TACAIDS akitoa burudani kwa washiriki wa changamoto hiyo.
Kampuni ya Acacia ,wamiliki wa Migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ni miongoni mwa kampuni ambazo zimekua zikitoa michango yao kusaidia kampunu ya GGM katika mapambano ya vita dhidi ya Ukimwi ambapo wafanyakazi wake pia ni miongoni mwa wanaharakati waliopanda Mlima Kilimanjaro.
Naibu Spika Dkt Ackson akisalimana na Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika ,Dkt Ackson kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima.
Zoezi la kupanda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika ,Dkt Tulia Ackson ,Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.
Zoezi la kupanda lilianza huku mvua ikinyesha,
(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini).
Reactions:

0 comments:

Post a Comment