Friday, 16 June 2017

1
Wazazi wakiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na watoto wao waliozaliwa kabla ya muda wakipatiwa huduma mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika. 
Maadhimisho hayo yamefanyika kitengo cha watoto njiti katika hospitali hiyo.
…………………….
 
Dar es salaam                                                     
Asilimia 98 ya watoto wanaozaliwa kabla ya siku na kutunzwa katika kitengo cha watoto walipo kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wanatoka salama na wakiwa na afya njema.
Hayo yamesemwa LEO na Muuguzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Rose Mathew  alipokuwa akizungumza na wazazi ambao wamefika Kiliniki na kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwenye kitengo cha watoto ambao wapo kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care hospitalini hapo.
Amesema matunzo ya Kangaroo Mother care yamesaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya siku na kwamba kitengo hicho kilichopo MNH kimekua faraja kwa wazazi.
“Hospitali inapata faraja kwasababu matunzo ya Kangaroo Mother care yameonyesha mafanikio makubwa katika hospitali yetu ikiwa ni njia mbadala ya matunzo ya watoto  wanaozaliwa kabla ya siku’’ amesema Muuguzi Rose Mathew.
Kwa upande wao wazazi waliofika kilini hapo wametoa wito kwa uongozi wa hospitali kuendelea kuboresha huduma hiyo kwasababu kituo hicho ni cha taifa na kinahudumia watoto wengi.
Jumla ya watoto 47 waliokuwa kwenye matunzo ya Kangaroo Mother care leo  wamehudhuria kilinikini  wote wakiwa na afya njema .
Reactions:

0 comments:

Post a Comment