Wednesday, 14 June 2017


NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
WATU kadhaa wameuawa na zaidi wengi 50 kujeruhiwa kufuatia moto mkubwa ambao umezuka kwenye jengo la ghrorofa 24 Grenfell Tower la makazi ya watu jijini London, Uingereza leo Jumatano Juni 14, 2017.
Meya wa jiji hilo Mstahiki Sadiq Khan amesema idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na watu wengine ambao idadi yao haijajulikana wameuawa.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji jijini London, kimetuma kwa uchache wahandisi wa moto 40, magari ya kubeba wagonjwa, (Ambulance), zipatazo 20 na zaidi ya askari wa zimamoto na uokoaji wapatao 200.
Mwakilishi wa kikosi cha zimaoto na uokoaji jijini London amesema kuna idadi kubwa ya waliokumbwa na kadhia hiyo ya moto lakini amekataa kusema ni watu wangapi wameuawa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment