Monday, 5 June 2017

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye viwanja vya Majengo Manispaa ya Mosjhi mkoani Kilimanjaro leo Juni 5, 2017 ambapo mwanasiasa wa upinzani, mbunge mstaafu wa CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro, marehemu mzee Philemon Ndesamburo (82), maarufu kama "Ndesa pesa" aliagwa. Maelfu ya watu walijipanga kwenye barabara za Manispaa hiyo, wakati gari lililobeba jeneza la mwili wa hayati Ndesamburo aliyefariki ghafla wiki iliyopita.Mrehemu Ndesamburo atazikwa nyumbani kwake eneo la KDC Kiborloni majira ya saa 7 mchana.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili atika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.   

  

  
Reactions:

0 comments:

Post a Comment