Friday, 16 June 2017

8
Profesa Samwel Manyere, Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza katika hafla ya kuwatunuku zawadi wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2015 na kidato cha sita mwaka 2016 waliofanya vizuri sana kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia jijini Dar es Salaam Juni 16, 2017.
01
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari akizungumza katika hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia Wanafunzi na Waalimu wao waliofanikiwa kufanya vizuri zaidi katika masomo ya Kemia na Baiolojia kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2015 na kidato cha sita mwaka 2016 iliyofanyika leo katika makao   makuu ya Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali Ocean Road jijini Dar es salaam.
1
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari akikabidhi zawadi kwa Mwanafunzi Congcong Wane wa shule ya sekondari Fedha  katika hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia Wanafunzi na Waalimu wao waliofanikiwa kufanya vizuri zaidi katika masomo ya Kemia na Baiolojia kwenye mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2015 na kidato cha sita mwaka 2016 iliyofanyika leo katika makao makuu ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)Ocean Road jijini Dar es salaam, Congcong pia ndiye mwanafunzi aliyefauru vizuri kitaifa katika somo la Kiswahili na ana uwezo mkubwa wa kuongea kiswahili, wa pili kutoka kushoto ni Samwel Manyere na wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassapa.
2
Mwanafunzi Congcong Wane wa shule ya sekondar Fedha akihijiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Swahili Steven Mumbi mara baada ya kupokea zawadi yake.
34
Wanafunzi wengine pia wakipokeza zawadi zao.
5
6
Wakurugenzi na mameneja wa Wakala wa Mkemia mkuu wa Serikali (GCLA)wakiwa katika hafla hiyo
7
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne na sita kutoka shule mbalimbali nchini waliofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia wakiwa katika hafla hiyo.

9
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
10
Baadhi ya walimu na wazazi waliohudhurika katika hafla hiyo
11
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassapa akimkaribisha mgeni rasmi Profesa Mohamed Bakari  ili kuzungumza katika hafla hiyo.
  13
Mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia akitoa shukurani kwa Mkemia mkuu wa Serikali kwa kuwatambua na kuthamini juhudi zao kutokana na kitondo cha kuwazawadia wanafunzi hao.
14
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Wakala wa Mkemi Mkuu wa Serikali Profesa David Ngassap, Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa  Samwel Manyere wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliozawadiwa kuangalia picha zaidi shuka chini.
151617
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa  Samwel Manyere akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa wakala huo mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwakabidh zawadi wanafunzi hao.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment