Tuesday, 6 June 2017

unnamed
 Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto, (kulia), akiwania mpira na Amani Kyata, wa Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Juni 6, 2017. Simba imetolewa kwenya michuano hiyo kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya kwenda suluhu na Nakuru All Stars katika muda wa kawaida.
1
Beki wa Nakuru All Stars, Amakanji Ekuba, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba Sc, Juma Luizio, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
2
Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio (kulia) akichuana na Beki wa Nakuru All Stars, Amakanji Ekuba, wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
3
Beki wa Simba, Mwambeleko Jamal (kushoto) akiwania mpira na beki wa Nakuru All Stars, Nandwa Sosi,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
4
Beki wa Nakuru All Stars, Mukhwana Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Juma Luizio,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
6
Beki wa Nakuru All Stars, Mukhwana Sadicky, akiondoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Juma Luizio,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
7
Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa Nakuru,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
8
Winga wa Simba, Jamal Mnyate, (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
9
Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto, akijipinda kupiga shuti kuelekea langoni kwa wapinzani, Nakuru All Stars,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
10
Beki wa Nakuru All Stars, akiokoa mpira wa hatari mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim,  wakati wa mchezo wa mashindano ya SportPesa Super Cup, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Picha kwa hisani ya Montage Ltd
…………………………………….
Mchezo wa pili wa Michuano ya SportPesa umemalizika kwa Nakuru All Stars kuibuka na ushindi wa jumla ya penalti 5-4 mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo hayo timu ya Nakuru inayocheza Ligi daraja la kwanza nchini Kenya imetinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Goriamahia pia ya Kenya ambayo ilifuzu baada ya kuifunga Jang’ombe boys ya Zanzibar mabao 2-0.
Michuano hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa mechi mbili kupigwa mchezo wa mapema utawakutanisha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga watakaocheza na AFC Leorpads ya Kenya na mchezo wa pili utakuwa kati ya Goriamahia na Nakuru All Stars. Kenya wameingiza timu tatu kwenye nusu fainali na bingwa wa michuano hii atacheza na Everton ya Uingereza Julai 13 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment