Sunday, 11 June 2017

*MBUNGE WA UKONGA ATOA MREJESHO WA TAARIFA YA KIKAO CHA BUNGE LA JMT NA KUTOA TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA JIMBONI UKONGA KWA WANANCHI*

Mbunge wa Jimbo la Ukonga ambae pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, Mhe. Mwita Waitara, amefanya mikutano miwili ya hadhara siku ya jana Jumamosi 10 Juni 2017, katika Kata ya Kivule na Kipera Ukonga.

Katika mikutano hiyo, Mhe. Waitara ametoa mrejesho wa taarifa kutoka kikao cha Bunge la JMT pamoja na hoja na taarifa mbalimbali zilizowasilishwa Bungeni ikiwemo Bajeti mpya ya serikali ya 2017/18 na ukweli wake kama ni kweli itamsaidia Mtanzania wa hali ya chini au itamkandamiza zaidi?

Katika mikutano hiyo, Mhe. Waitara amepokea kero mbalimbali za wananchi katika maeneo yao na kuzitolea ufafanuzi, akielezea mradi wa barabara ya Kitunda relini ambayo itajengwa kwa kiwango cha changarawe na barabara ya Moshi bar ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami, pamoja na taarifa miradi yote inayoendelea Jimbo la Ukonga, kwa zile zilizopo nje ya uwezo wake amezichukua na kuzipeleka Halmashauri, Serikalini na Bungeni.Leo Jumapili 11 Juni 2017 Mhe. Waitara atafanya mkutano mwingine wa hadhara katika mtaa wa Machimbo, miingoni mwa wageni watakaohudhuria mkutano huo  leo ni Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule au Profesa Jay na Mbunge wa Ubungo; Mhe. Saed Kubenea ambae pia na Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani.

Pia atakuwa Mubashara kupitia ukurasa wake wa face book mfuate "Mwita Waitara"
Reactions:

0 comments:

Post a Comment