Sunday, 25 June 2017

 MBUNGE wa Jimbo la Tanga
(CUF) Alhaji Mussa Mbaruku amewataka wananchi heri ya sikukuu ya Eid
El Fitri huku akiwataka kujiandaa na ujio wa fursa ya mradi wa bomba la mafuta
ghafi kutoka hoima nchini Uganda
hadi Bandari ya Tanga kwa kuongeza uzalishaji.

Alhaji Mussa aliyasea hayo wakati akizungumza na mtandano huu ambapo alisema mradi huo ni mkubwa ambao utahusisha watu wengi hivyo wananchi wanapaswa kujipanga ili kuweza kuendana na fursa hiyo muhimu kwa ajili ya kujiongezea kipato halisi.Alisema lazima wakazi wa mkoa
huo watambue kuwa wakati mradi huo ni mkubwa ambao unaweza kuchangia ukuaji wa
kipato chao hivyo wajiandae kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mama
ntilie waweze kuendesha shughuli zao kisasa.

“Mkoa wa Tanga hasa kwenye
Jimbo langu la Tanga mjini kutatekelezwa mradi mkubwa wa mradi wa boma la
mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hiyo
wananchi wangu wajiandae kwa kuongeza uwajibika na uzalishaji ambao utakuwa na
tija kwao “Alisema.

“Lakini pia niwaambie wenzetu
madereva wa tax, mafundi wajiandae kikamilifu kuona namna ya kuboresha huduma
zao kwani ujio wa mradi huo utalifanya Jiji la Tanga kuwa na watu wengi kutoka
maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuweza kupata mafanikio
“Alisema.

Aidha pia mbunge huyo aliwataka
waumini ya dini ya kislaam kuendelea kutenda mema hata baada ya kumalizika
mwezi mtukufu wa ramadhani ikiwemo kuwajali wengine.

Mbunge huyo pia aliwataka
wananchi wa Jimbo hilo
kuhakikisha wana sheherekea vema sikukuu ya Iddi Salama kwa kuwa makini hasa
wakati watoto wao wanapokwenda kutembelea wawe na
wasaidizi.

 Habari kwa hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha

Reactions:

0 comments:

Post a Comment