Tuesday, 6 June 2017

MBUNGE wa Mafinga mjini, mkoani Iringa, Mhe. Cosato
Chumi, (kushoto) na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga, Charles Makoga, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa utoaji huduma wa gari la kubebea wangonjwa la kituocha afya cha Igohole. Gari hilo limenunuliwa na mbunge Chumi.
MBUNGE wa Mafinga mjini, Mhe. Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya kituo cha afya cha Igohole, wilayani Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo hilo.
Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilikabidhiwa kwa
uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa kituo hicho katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Igohole, mjini Mafinga.
Akikabidhi msaada huo Mhe. Chumi alisema;
“napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. uadilifu na uaminifu kwa serilikali ndio umetufanya tushirikiane vyema katika
mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”Alisema.
Alisema gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati mgonjwa akipelekwa hospitalini.
Baada ya kukabidhi gari hilo, Mhe. Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha jimbo la mafinga
mjini linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa kupokea msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa lilotelewa na mbunge wa Mafinga Mjini, Mhe. Cosato Chumi kwa kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Habari, Picha na Fedy Mgunda)


Reactions:

0 comments:

Post a Comment