Tuesday, 20 June 2017

Mtaalamu Mbobezi wa masuala ya Afya na Kazi kutoka MUHAS jijini Dar es Salaam, Bw.Yahya Kishashu, akitoa mada kuhusu namna madaktari wanavyoweza kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyeumia mahala pa kazi. Mada hiyo ameitoa leo Juni 20, 2017 wakati wa siku ya pili ya mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa madaktari wa hospitali za jijini Dar es Salaam ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepatwa na madhara hayo kutokana na kazi aifanyayo.
Mkurugenzi wa huduma za afya na tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, (aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo wakati wa mafunzo hayo
Dkt. Abdulsalaam (kulia), akizungumza na Dkt. Gershom Phanuel Ruyanga, wakati wa mapumziko ya mafunzo hayoDkt. Hussein Mwanga kutoka MUHAS, akitoa mada

Daktari Bingwa wa upasuaji mifupa na majeruhi kutoka Taasisi ya Mifupa MOI ya jijini Dar es Salaam, Dkt.Robert Mhina, akizungumza mbele ya madaktari hao wakati wa mafunzo hayo
Mtaalamu Mbobezi wa masuala ya Afya na Kazi kutoka MUHAS jijini Dar es Salaam, Bw.Yahya Kishashu, akizunguzma
Mshiriki wa mafunzo akitoa maoni yake
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo
Reactions:

0 comments:

Post a Comment