Saturday, 3 June 2017


NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
SIKU moja kabla ya pambano la fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2017, almaarufu kama UEFA Champions League, kocha mkuu wa Real Madrid, Mfaransa, Zinedine Zidane, alimwagia sifa lukuki Mshambuliaji wake kutoka Ureno, Christiano Ronaldo, kuwa anajua kulisakata kabumbu pengine kuliko yeye (Zidane) wakati akicheza na kwamba anaamini Ronaldo ataiongoza vema safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuibuka mshindi na kutwaa kombe hilo dhidi ya Juventus ya Italia, usiku wa kuamkia leo Juni 4, 2017 mjini Cardiff, Wales..
Ama kwa hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa, Christiano Ronaldo, akipachika mabao mawili,Casemiro bao moja na Marco Asenso bao moja na hivyo Madrid kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1, bao la Juventus lilipachikwa wavuni na Mandsukic, ambaye alifunga bao zuri la ksuawazisha.
Ushidni huo unaifanya Madrid, kuwa timu ya kwanza barani Ulaya kufanikiwa kulitete taji lake la mabingwa Ulaya na Juventus kwa mara ya kwanza inakubali kipigo kikubwa cha mabao katika mchezo wa fainali katika historia yake.
Hata hivyo mshambualiaji wa Juventus, alilambwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya njano mara mbili kwa kumchezea vibaya tena kwa makusudi, mlinzi Sergio Ramos na hivyo kuwalazimu kucheza pungufu uwanjano japo kwa dakika chache za kipindi cha lala salama.Reactions:

0 comments:

Post a Comment