Wednesday, 14 June 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thorntonalipofika Ikulu kwa Mazungumzo, kulia ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles June 14, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton alipofika Ikulu kwa Mazungumzo June 14, 2017

Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu June 14, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation  Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017. wakiwa na  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton pamoja na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mhe. Ian Myles balozi wa Canada Nchini pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton alipofoika ikulu kwa mazungumzo juni 14,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi  baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton  Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017. 


3
Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema Kampuni ya madini ya Acacia imekubali kufanya mazungumzo na Serikali ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo Serikali inaidai kwa kufanya shughuli zake hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation inayomiliki kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton leo Ikulu jijini Dar es Salaama, Rais Magufuli amesema kampuni ya Barrick imekubali  mazungumzo na Serikali ya Tanzania na kulipa  fedha wanazodaiwa.
 “Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini kwa maslahi ya pande zote mbili” alisema Rais Magufuli
Rais Magufuli alisema kuwa licha ya kampuni hiyo kukubali  kulipa fedha wanazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu  hapa nchini.
Nae, Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo inatakiwa kulipa kwa Serikali ya Tanzania.
Mazungumzo hayo kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kampuni ya Acacia yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini  Ian Myles na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi
Reactions:

0 comments:

Post a Comment