Wednesday, 21 June 2017


KEM
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
RAIS dk.John Magufuli ,amezindua kiwanda cha vifungashio (global packaging co. ltd)kilichogharimu bil.8 ,na kiwanda cha kutengeneza nondo cha Kiluwa chenye thamani ya bil.200 ,vilivyopo Kibaha,Pwani.
Aidha amekemea baadhi ya taasisi zinazoweka mazingira ya rushwa na urasimu wakati wa kutoa vibali kwa wawekezaji ikiwemo OSHA,NEMC na shirika la viwango TBS.
Dk.Magufuli ,pia amezitaka taasisi za kifedha kukopesha watanzania wazalendo na wale wenye nia ya kuwekeza kwa manufaa mapana ya taifa.
Hayo aliyasema wakati akizindua viwanda vya global packaging ,cha nondo -Kiluwa na kuzindua na kufungua kiwanda cha kuunganisha matrekta ya Ursus .
Dk.Magufuli ,alisema ukosefu wa dhamana kwa wawekezaji linadidimiza kasi ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya ukuaji wa uwekezaji na ujenzi wa viwanda .
Rais Magufuli ,alieleza kwamba ,suala la vibali ameliona na anataka asikie kuna mwekezaji amebaniwa kibali ,ili amshughulikie .
“Hili nilishaliona ndio maana vibali vya NEMC ,vimefutwa na kupitishwa na bunge katika bajeti 2017/2018 ” alisema dk.Magufuli .
Dk.Magufuli alielezea kuwa ,kuna mabank zaidi ya 53 yalikuwa hayakopeshi wawekezaji ,yalizoea kufanya biashara na serikali huku wenye madaraka na wakubwa walikuwa wakitumia vibaya upenyo huo .
“Serikali ilikuwa inajila yenyewe ,nilipozibana ,kama Tanesco nilizuia ,bima ya afya na nyingine ,wakashtuka nikajua aaah nimegusa penyewe “
Aliipongeza bank ya TIB kwa kuamua kuikopesha kiwanda cha vifungashio ,alimpongeza mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo ,kwa kasi anayoenda nayo na waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage.
Dk.Magufuli alisema ,kutokana na upungufu wa vifungashio kiwanda hicho ,kitasaidia wavuvi ,wazalishaji wa madini ,viwanda na wakulima kununua kwa gharama nafuu ndani ya nchi .
Alisema soko la vifungashio lipo ,ndani ya SADC ,Tanzania na nje ya nchi na ataendelea kukiunga mkono kiwanda hicho .
Akizindua kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus ,rais huyo ,aliitaka NDC iwe mpya yenye kutoa matunda kitaifa ,sasa inafanya kazi na kuondoa ndoto yake ya kuifuta kwani inaenda kwa kasi yenye matumaini .
Dk.Magufuli alisema  mradi wakuunganisha matrekta ameubeba kwani yatasaidia wakulima.
” Kilimo ni shughuli inayofanyika kwa asilimia 80,wananchi wanategemea kilimo ,wengi wanatumia kilimo cha jembe la mkono hivyo matrekta itasaidia kupunguza tatizo hilo.”alisema.
Kwa mujibu wake ,waangalie bei tofauti na matrekta yanayoagizwa nje ya nchi ili yaweze kununuliwa na watanzania .
Alisema wakopeshwe wakulima kwa gharama nafuu . 
Alieleza kwamba ,serikali imeanza kutoa utitiri wa kodi kwa asilimia 80 za kilimo ,asilimia 7 kwenye ufugaji na tano kwenye uvuvi ili viwe na mvuto na kuendelea na biashara .
Alisema eneo la pembejeo limeoza na wameanza kulifuatilia,kuna pembejeo hewa ,madudu ndani ya pembejeo wengine walishakufa wala hawana mashamba lakini wameandikiwa wamepata pembejeo hizo.
 “Tutatoa hatua ,hatujanyamaza ,hewa ni nyingi ,wapo walioandikishwa watu hewa 56,000 Tasaf na pembejeo wapo ” sitolivumilia”
Hakusita kusema Tanzania ina urafiki mkubwa na nchi ya Poland na amewahakikishia Tanzania ni sehemu nzuri ya  uwekezaji .
Akizindua kiwanda cha chuma cha -Kiluwa ,aliwaomba wataalamu wa wizara kuangalia kwa faida pana uwezekano wa kutumia chuma iliyopo nchini kuliko kununua nje .
Alimpongeza Mohammed Kiluwa kwa kuzalisha nondo yenye kiwango na kuungana na wawekezaji wa kichina.
Lakini aliitaka wizara husika na wawekezaji kununua chuma Liganga na Mchuchuma maeneo yaliyopo nchini kuliko kununua China .
Katika hatua nyingine ,aliwaasa wawekezaji ,kujali maslahi ya wafanyakazi na mikataba yao .
Dk.Magufuli, alisema wafanyakazi ndio wanaoongeza mali ya wenye mali hivyo ni lazima kuwapa motisha ili wafanyekazi kwa bidii .
Nae waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji ,Mwijage ,alisema nchi nzima ina viwanda vya vifungashio 20 mojawapo ikiwa global packaging .
Alisema mkoa wa Pwani ,unaongoza kwa viwanda mbalimbali nchini ,ikiwemo vitano anavyovizindua ,kufungua katika ziara yake .
Mwijage alieleza kuwa ,kujenga na kulinda viwanda ni majukumu yaliyochini yake na anaahidi kuvilea .
Alisema ,viwanda hivyo vitawezesha ajira hasa kwa vijana na kuongeza pato la Taifa .
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa ,alisema barabara ya Mzenga -Makofia ni kero kubwa hivyo aliomba kuangaliwa kwa jicho la karibu iwe kwa kiwango cha lami .
Alisema barabara hiyo itarahisisha usafiri kwa kiasi kikubwa .
Jumaa alieleza kuwa ,wawekezaji wakifika eneo lolote wanaangalia miondombinu ya barabara .
Mbunge huyo ,alisema anasumbuliwa na wananchi ,km .5 ambayo ni ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni .
Alimuomba rais kuangalia kwa namna ya pekee Kituo cha afya cha Mlandizi ,kipandishwe hadhi kuwa hospital ya wilaya .
Jumaa alisema ameshaanza kujenga uzio wa utakaogharimu Mil.200 ambao utasaidia kusukuma kigezo cha kupandishwa hadhi kituo hicho .
Awali ,mwanzilishi wa kiwanda cha global packaging, Joseph Wasonga ,anasema kiwanda kipo ubia na NDC ambapo kiwanda kina asilimia 94 .
Alisema kiwanda hicho kwa mwaka kitazalisha vifungashio milioni.16 . Wasonga alitaja changamoto ya ukosefu wa dhamana kwa wawekezaji unapofikia hatua ya kwenda taasisi za kifedha ,riba kubwa na tatizo la vibali .
Wasonga ,aliishauri serikali na bank kuu kusimamia suala hilo ili kuwapunguzia makali wawekezaji.
Alisema kwasasa wameshaajiri wafanyakazi 110 kati yake 109 ni wazawa ,malengo yao ,ni kuzalisha mara mbili ya sasa .
Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa,Mohammed Kiluwa alimwambia Rais,mkoa huo,umejipanga kujiinua kiuchumi .
Aliomba kwa rais ,kupewa ardhi nyingine ili aweze kujenga viwanda vitano kwa kushirikiana na marafiki zake wa kichina.
Kiluwa alisema,mradi huo mkubwa utazalisha zaidi ya tani 2,000 na kuajili watu 300-800.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment