Wednesday, 28 June 2017

kigom
Jaji Kiongozi Mahakama  Kuu ya Tanzania, Mhe, Ferdinand Wambali  wa akisalimiana  na baadhi ya  watumishi  wa Mahakama ya Wilaya  ya Kasulu   mara baada ya kuwasili katika Mahakama hiyo hivi karibuni, wakati alipotembelea  Mahakama hiyo na kufanya ukaguzi  wa shughuli za utendaji kazi   na miundombinu ya Mahakama.
……………………………………………………………………………
 Na Magreth Kinabo  – Mahakama ya Tanzania
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinad Wambali  amesema kwamba mkoa wa Kigoma utapatiwa Mahakama  Kuu hivi karibuni,ikiwa ni hatua ya kuwaondolea  adha wanaoipata wananchi ya kutafuta huduma ya mahakama  hiyo kutoka eneo moja hadi jingine
Kauli hiyoimetolewa tarehe mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Kiongozi wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya Kibondo kuhusu malengo ya ziara yake katika mkoa wa Kigoma,hivyo aliwataka  baadhi  ya viongozi  na  wananchi kuvuta subira.
Jaji Kiongozi , pia alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mahakama Kuu  Kanda  ya Tabora, wakiwemo baadhi ya watumishi wa Mahakama  Kuu kutoka  kanda hiyo  ambayo inajumuisha mikoa miwili yaani na Tabora na Kigoma.  
“Tayari kiwanja kimeshapatikana na eneo la Buhigwe  na tenda imeshatangazwa, hivyo mchakato wa ujenzi utaanza hivi, karibuni,”alisema Jaji Kiongozi.
Kiwanja  hicho kina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 16,000.
Mkoa  huo, unahitaji  huduma ya Mahakama Kuu  kwa sababu ya kukua kwa   idadi ya watu,pia hivi sasa watu wanatoka  katika mkoa  huo  kwenda kufuata  huduma za Mahakama Kuu mkoa wa Tabora , pia kukua  kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
Jaji Kiongozi   aliongeza katika kanda hiyo, wilaya ambazo hazina   mahakama za wilaya zitajengewa mahakama kwa kuwa Mahakama  ya Tanzania kupitia mpango Mkakati wa Miaka Mitano(2015/16 hadi  2019/20 imejipanga kujenga mahakama kila wilaya, tarafa na kata.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment