Monday, 5 June 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Mhe. Sophia Mjema akiwasili kwenye chuo cha St. Mark kilichoko Buguruni-Malapa Juni 5, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni-Malapa jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017. Mhe, Mjema lifanya ziara ya kikazi chuoni hapo. Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chrispin Makota.

NA DICKSON MULASHANI
Mkuu wa wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, Mhe. Sophia Mjema, amesema mkakati wa kusambaza huduma ya  intaneti (WIFI) katika vyuo vikuu wilayani kwake  unaendelea kwa kasi na umesimama kwa muda kutokana na hali ya mvua lakini baada ya hali hii kila kitu kitakuwa kama ilivyoahidiwa, lazima msome kisasa” alihitimisha mama Mjema.
Pia mkuu wa wilaya Mhe. Mjema amekipongeza chuo cha St Mark (chuo kikuu kishiriki cha St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.
“Nimekuja kuwaona kwani nauthamini sana uwepo wenu katika wilaya yangu (Ilala)." Alisema.
Mhe. Mjema alitangza kufungua milango ya fursa kwa wasomi hao kufika ofisini kwake na kuleta mawazo pamoja na nguvu zao na kwa kushirikiana na wataalamu wa ofisi yake ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele huku akikazia suala la uzalendo pamoja na wito wa Mh Rais Magufuli kuhusu kufanya kazi.
Nae Rais wa chuo kwa niaba ya wanafunzi wote alifikisha Changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la mikopo pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwani limekuwa likidhohofisha maendeleo ya taaluma alitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya na kuahidi ushirikiano na ofisi ya wilaya pamoja na kujitoa kutumia taaluma zao ndani ya jamii kwa ujumla.
Akihitimisha zoezi hili pamoja na kumshukuru Mhe.Mjema kwa kufika chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa Chuo alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Chuo hicho hasa wakati huu ambapo milango ipo wazi kwa wanafunzi kudahiliwa vyuoni moja kwa moja huku akiwaondoa hofu wale wanaobanwa na kazi kuwa watapata fursa ya kusoma masomo ya jioni.
Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mhe.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Mark Dkt.Peter Kopweh akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya alipokuwa akizuru maeneo mbalimbali katika chuo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji Ilala Bw. Benjamin Chagula wakati akiangalia namna ya kutatua Changamoto ya mipaka ya chuo hicho inaingiliwa na wananchi wanaoishi eneo jirani.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment