Sunday, 11 June 2017


NA K-VIS BLOG, UWANJA WA TAIFA
MASHINDANO ya 18 ya kuhifadhi Quran tukufu kwa mataifa ya Afrika, yanafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na kufikia saa 4;30 asubuhi, tayari uwanja huo wa Taifa wenye uwezo wa kuchukua watu elfu 60 ulikuwa umejaa.
Kufuatia hali hiyo, mratibu wa mashindano hayo, Sheikh Nurdin Kishki, (pichani juu), alilazimika kusimama na kutoa tangazo kuwa , kutokana  na sababu za kiusalama, uwanja huo tayari umejaa pomoni na kuwataka waislamu na wananchi wengine ambao bado walikuwa wanaendelea kuwasili kubaki  nje ya uwanja na tayari skrini kubwa imeandaliwa kwenye gari kubwa nje ya uwanja na hivyo watu wanaweza kufuatilia mashindano hayo kupitia runinga.
Sheikh Kishki alimuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi, kuruhusu msimu ujao wa mashindano hayo, vitumike viwanja vyote viwili yaani ule mkubwa wa taifa na ule ulio jirani wa Uhuru.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya Alhikma Foundation yamewaleta pamoja vijana wa kiislamu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

 Sehemu ya umati wa wasilamu waliofika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 11, 2017 kushuhudia fainali za mashindano ya 18 ya kuhifadhi Quran tukufu kwa mataifa ya Afrika

 Mshiriki toka Burundi, Zaidi Niyitunga
Jopo la majaji
Reactions:

0 comments:

Post a Comment