Thursday, 15 June 2017NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIONGOZI wa muda mrefu wa Shirikisho la Mpirawa Miguu nchini, (TFF), Alhaji Ahmed Iddi Mgoyi, (pichani), ametangaza “kung’atuka kwenye nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo na kwamba huu ndio muda wake wa mwisho na hatagombea tena kwenye uchaguzi ujao.
Mgoyi ambaye anawakilisha mikoa ya Kigoma na Tabora amekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kwa takriban miaka 13 mfululizo ameweka historia ya kuwa mjumbe mwenye umri mdogo kuliko wote pale alipogombea kwa mara ya kwanza ujumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF.
Alhaji Mgoyi katika taarifa yake aliyoitoa Juni 13, 2017 amesema, “Pamoja na kuwa bado nina nguvu uwezo na sifa za kuendelea kugombea lakini pia nimeamini ni wakati wa kutoa nafasi pana zaidi kwa wengine kugombea na kuwa badala yangu na heshima kwa fikra nyinginezo. Na ninaondoka nikiwa mjumbe wa muda mrefu zaidi ya wote kwenye Kamati ya Utendaji inayokamilisha kipindi cha kikatiba na kwa dhati kabisa naamini kwenye kutoa nafasi kwa wengine.” Amesema  Alhaji Mgoyi.
Aidha Alhaji Mgoyi ambaye pia ameweka rekodi ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwa muda mrefu zaidi kuliko wajumbe wote waliopo sasa, amewaomba radhi wale wote ambao wangependa au kutarajia kuwa angewania tena nafasi hiyo.
Kama sehemuya familia ya mpira wa miguu, Alhaji Mgoyi amewashkuru kwa imani yao kwake na bado yupo nao pamoja.
Hata hivyo Alhaji Mgoyi ametoa angalizokwa wale wagombea wote wanaoomba kuendelea na wapya watakuwa wamejiuliza mara za kutosha, wamejipima vya kutosha na kuzihakiki dhamira zao, wamejiridhisha na wanavyoijua TFF, ukubwa wake na shughuli zake, wamefuatilia na kutambua vema mahitaji ya mpira wetu, wametathmini changamoto, madhaifu na makusudi ya kiUongozi na wapo tayari kwa mabadiliko, wametambua maeneo TFF inayofeli au hayajafanywa vema zaidi na wanaamini kwenye kuwa sehemu ya ufumbuzi, wamezikataza nafsi zao kufuata matamanio ya mapenzi ya timu zao, wanafahamu nguzo kuu za mpira wa miguu na changamoto zinazozikabili na namna ya kuzitatua, utayari wao kujitolea kwa hali na mali, kuheshimu miiko ya kiuongozi na kuimarisha nidhamu na Uadilifu.
Nimesukumwa kutoa Ushauri wangu huu kwa kuendelea kuathiriwa na kutoamini sana kwenye Utekelezaji na Udhibiti wa  kimfumo wa kupatikana kwa Viongozi wa Mpira.. hasa katika ngazi za juu kama hizi zinazokwenda kugombewa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment