Saturday, 13 May 2017

  MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Yanga, wanakaribia kulinyakua tena kombe hilo baada ya "kula kiporo" kingine kwa kuibanjua Mbeya City mabao 2-1 katika pambano lililopigwa leo Mei 13, 2017 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imerejea kileleni baada ya kufikisha pointi 65 sawa na mtani wake wa jadi Simba, lakini ikiwa mbele kwa faida ya mabao ya kufunga. Lakini pia Yanga bado inacho kiporoo kingine kimoja dhidi ya Mbao FC ya Mwanza. Simba imebakiza mchezo mmoja wakati Yanga imebakiza michezo miwili hali inayoonyesha wazio kuwa  njia ya ubingwa kwa Yanga iko wazi, endapo itafanikiwa kushinda michezo yake yote miwili iliyobaki. Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa (kushoto) akimkalisha beki wa Mbeya City Tumba Lui, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Simon Msuva katika dakika ya 7 na Obrey Chirwa dakika ya 64, huku bao la kufutia machozi ya Mbeya Citylikifungwa na Haruna Shamte. 
Tambe akimiliki mpira katikati ya mabeki wa Mbeya City, wakati wa mchezo huo.(PICHA NA MAFOTO BLOG)
Reactions:

0 comments:

Post a Comment