Wednesday, 3 May 2017


Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, (wapili kulia), na viongozi wengine, walionyesha nakala ya  “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016” wakati wa uzinduzi wake uliokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyobo vya habari duniani uliofanyika kitaifa jijini Mwanza.
21
Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, ambaye amemwakilisha Rais John Pombe Magufuli.

#BMGHabari
Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza hii leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia), akizindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016”. Kushoto ni mjumbe bodi ya Misa Tanzania, Lilian Lucas.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016”.
Uzinduzi wa “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari kwa mwaka 2016”.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, leo amezindua “taarifa ya hali ya vyombo vya Habari nchini Tanzania kwa mwaka 2016” kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza.

Akizungumza mapema kabla ya uzinduzi huo, Dkt.Mwakyembe, ameahidi kutetea na kulinda uhuru wa waandishi wa habari hususani wanaoandika habari za uchunguzi huku akiwahimiza waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi badala ya habari za kihisia.


Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, amebainisha kwamba taarifa hiyo imeangazia tathmini ya vyombo vya habari kuanzia Januari Mosi hadi Disemba 31, 2016 ambapo imezinduliwa katika nchi 11 wanachama wa SADC.

Katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC),leo Mei 3,2017 imefanya mkutano na wadau wa habari mkoani Shinyanga kujadili namna klabu hiyo ilivyo na wajibu wa kuendeleza amani katika jamii.
Mgeni rasmi katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga.
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe 3 mwezi Mei ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho ya kitaifa kufanyika kitaifa jijini Mwanza,lakini yamefanyika pia katika kila mkoa nchini yakiwa na kauli mbiu inayosemayo “Klabu za Waandishi wa Habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii”.
Awali akitoa hotuba yake,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde alisema Klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii hivyo kuwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazojenga utaifa na kuleta mshikamano katika jamii.
Malunde alisema Klabu za waandishi zinawaweka pamoja waandishi wa habari hivyo kupitia umoja huo zinawabijika kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza amani katika jamii kwani pasipo na amani hakuna maendeleo.
Aliongeza kuwa kutokana na nguvu ya vyombo vya habari,amani katika jamii itaendelea kuwepo endapo tu waandishi wa habari watazingatia maadili ya kazi yao na kuepuka kushabikia mambo yasiyo na maana.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack aliwataka waandishi wa habari kutanguliza utanzania na uzalendo katika habari wanazoandika.
“Ndugu zangu waandishi wa habari mnajukumu kubwa la kulinda amani ya nchi hii,tumieni kalamu zenu vizuri,epukeni kuandika habari za kujenga hofu na mnapoandika basi msiegemee upande mmoja,sikilizeni hata upande wa pili ili kutenda haki”,alieleza mkuu wa mkoa.
Katika hatua nyingine Telack aliwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano walionao na kujiendeleza kielimu huku akiwashauri kuanzisha miradi itayowakomboa kiuchumi kwani fursa mbalimbali za kiuchumi zipo mkoani humo.
“Nitoe wito kwa waandishi wa habari kuunga mkono sera ya uchumi wa viwanda,andikeni habari kuhusu viwanda na kilimo na kupitia umoja wenu anzisheni mashamba ya pamba na alizeti na mnao uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo ili kuinua uchumi wenu,andikeni proposal mnaweza kuanzisha hata kiwanda cha maziwa”,aliongeza Telack.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akifungua mkutano wa wadau wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ngazi ya mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde
Katikati ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack
Wa kwanza kulia ni  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akifuatiwa na Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3,2017
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa hotuba ukumbini
Wadau wa habari wakiwa ukumbini
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi akisisitiza jambo ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Mwandishi wa habari Suleiman Shagata akichangia hoja ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde(kushoto) na katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiongoza majadiliano ukumbini
Kaimu Mwenyeti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Shaaban Alley akizungumza ukumbini
Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Nunu Abdul akiandika dondoo muhimu
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Wadau wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini
Msaidizi wa Askofu Kanisa kuu la KKKT Shinyanga Usharika wa Ebenezer Trafaina  Assery Nkya akizungumza ukumbini
Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza ukumbini
Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akizungumza ukumbini
Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga akichangia hoja ukumbini
Mdau Gelard Ng'ong'a kutoka shirika la Rafiki SDO
Afisa habari kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji wa Kahama (KUWASA) bwana Mkama akichangia hoja
Mdau wa habari bwana Chief Abdallah Sube akichangia hoja
Bwana John Myola kutoka Shirika la AGAPE Shinyanga akizungumza ukumbini
Mkurugenzi Msaidizi Radio Faraja,bwana Anikazi Kumbemba akizungumza ukumbini
Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga,Bi Alice Mazoko akichangia hoja 
Mwandishi wa habari Patrick Mabula akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack akizungumza ukumbini
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari. Picha zote kwa hisani ya Shinyanga Press Club
Reactions:

0 comments:

Post a Comment