Saturday, 6 May 2017
NA K-VIS BLOG, ARUSHA
WATU 37 wakiwemo wanafunzi 32 wamefariki dunia katika ajali ya basi wilayani Karatu leo Mei 6, 2017.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema, ajali hiyo pia imeua walimu watatu na dereva wa basi hilo mali ya shule ya msingi ya LuckyVincent Nursery and Primary School ya Kwa-Mrombo jijini Arusha.
Katika ajali hiyo iliyotokea baada ya basi hilo kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo la mto Malera kandokando ya barabara kuu ya Karatu, kata ya Rhotia wilayani humo, imeelezwa kuwa wanafunzi hao ni wa darasa la saba na walikuwa wakielekea Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wenzao wa shule ya Msingi Tumaini iliyoko wilayani humo.Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutoka kwa ajali hiyo mbaya na kwamba wanafunzi wengine wanne wamejeruhiwa na wamelazwa kwenye hospitali ya Lutheran mjini Karatu. Walimu wawili na dereva mmoja ni miongoni mwa waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo mbaya na ya kusikitisha.
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amin.

Naye Waziri Mkuu wa zamani, na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa katika salamu zake za rambirambi zilizotumwa mapema leo amesema“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali mbvaya sana iliyotokea leo asubuhi wilayani karatu, wanafunzi kadhaa na walimu wao wamepoteza maisha, ni ajali mbaya iliyoifanya siku hii iwe siku mbaya sana ktika historia ya nchi yetu, nawapa pole wote waliopatwa na maafa haya nawataka watanzania tusimame pamoja kusaidiana kwa jambo lolote tutakalopaswa kufanya wakati huu mgumu”
Nachjo chama cha ACT Wazalendo katika salamu zake za rambirambi,

 kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi, walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya awali na msingi ya Lucky Vicent ya Jijini Arusha, vifo vilivyotokana na ajali ya basi iliyotokea katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha
ACT Wazalendo katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Facebook tunatoa pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao, ndugu na jamaa waliopoteza walimu na wafanyakazi wa shule hiyo, pamoja na watanzania wote kwa ujumla. Pia tunawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapate kupona kwa haraka.
Mola awalaze pema watoto na ndugu zetu wote waliopoteza maisha katika ajali hii. Msiba huu ni wa Taifa zima.
majina ya wanafunzi waliofariki
Reactions:

0 comments:

Post a Comment