Sunday, 7 May 2017


NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
LEO Jumapili Mei 7, 2017, Wafaransa wataamua, kati ya kijana wa miaka….Emannuel Marcon na Mwanamama mwenye umri wa miaka 48, Marine Le Pen kuwa Rais wa  nchi hiyo.
Kiasi cha vituo vya kupigia kura 70,000 vimefunguliwa leo katika uchaguzi wa awamu ya bpili ili kuamua nani nkati ya wawili hao atakuwa mrithi wa Rais wa sasa, Francois Hollande.
Raundi ya kwanza ya uchaguzi huo uliofanyika Aprili 23, 2017 haukuamua mshindi, ingawa katika uchaguzi huo, Emmanuel Macron kutoka chama tawala cha Independent aliibuka mshindi wa kwanza kwa kupata asilimia 24.01 ya kura zote zilizopigwa na Mwanamama Marine Le Pen wa chama cha National Front, alipata asilimia 21.3 ya kura zote.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa Marcon atamshinda mpinzani wake ambaye sera zake za kutaka Ufaransa kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya na kupinga wahamiaji zimekuwa zikipingwa na Wafaransa wengi
Kwa upande wake Macron anataka kusimamia uchumi na kupanua ushirikiano wa Jumuiya ya Ulaya kinyume na sera za mpinzani wake.
Ni nani huyu Emmanuel Marcon?, Emmanuel Marconmwenye umri wa miaka 39, ni mfanyakazi wa zamani wa benki ya rasilimali, ambaye hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa.
Marcon ni waziri wa zamani wa serikali inayomaliza muda wake, Marcon amezaliwa na wanandoa ambao ni madaktari, amekulia katika mji wa Amiend na alisoma katika shule ya jimbo ya Jusuit kwenye mji alikozaliwa kabla ya kuhamia Paris na kuendelea na masomo na aliendelea kusoma masuala ya sayansi ya siasa shule ya Lycee Henri-1V.
Ni nani Marine Le Pen?
Marine Le Pen ameishi chini ya kivuli cha baba yake, Jean Marie Le Pen, mwanzilishi wa chama cha mfengo wa kulia cha National Front mnamo mwaka 1972. Chama ambacho amekuja kukiongoza miaka 40 baada ya kuanzishwa kwake.
Akiwa na umri wa miaka 48, Marine Le Pen tayari ameachika mara mbili, na ni mama wa watoto watatu na mara zote amekuwa akiomba vyombo vya habari, kuwa kando na masuala ya watoto wake kwani ni masuala binafsi zaidi.
Hata uhusiano na baba yake ni suala linguine ambalo limekuwa likijadiliwa sana na vyombo vya habari.

Mlipuko wa bomu kwenye nyumba ya familia yao huko Paris yeye akiwa na umri wa miaka 8 kumemfanya ajue fika kuwa Baba yake ni mpambanaji aliyesugu na hata baada ya wazazi wake kuachana, Marine Le Pen alitumia mjuda mwingi akiwa ofisini kwa baba yake.

Umahiri wake wa kuongea mbele ya hadhira, kulimfanya asomee sheria na mnamo mwaka 1998 na kuwa mshauri wa kisheria kwenye chama cha baba yake na kuendelea kukua katika Nyanja mbalimbali kwenye chama, na hadi kufikia cheo cha Makamu wa Rais na Mbunge wa bunge la Ulaya (European Union Parliament) na baadaye kuwa mbunge katika bunge la Ufaransa, na alijaribu kuregeza taswira ya chama chao katika jamii.
Hali hii ilizua mtafaruku na baba yake ambaye ni “msema ovyo”, na msuguano huo haukuisha hadi Marine Le Pen alipochukua madaraka ya uongozi wa chama mnamo mwaka 2011 na hapo alikuwa na fursa ya kukibadilisha chama anavyotaka.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment