Monday, 1 May 2017

 Baadhi ya wafanyaakzi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wakiungana na wenzao katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kiraifa yamefanyika kwenya uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
NA K-VSI BLOG/Khalfan Said
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wameungana na wenzao jijini Dar es salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi kwa matembezi kutoka Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru.

Kitaifa sherehe hizo zimeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mjini Moshi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi.”

Mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Bw. Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi na magari kadhaa kutoka taasisi za umma na binafsi yakionyesha huduma zitolewazo na taasisi hizo.
WCF ni Mfuko ulioanzishwa kwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 na ndio Mfuko unaowajibika kutoa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi walioumia, au kupatwa na maradhi yaliyoababishwa na kazi wanazozifanya lakini pia kutoa Fidia kwa wategemezi pindi Mfanyakazi anapofariki kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment