Wednesday, 10 May 2017

Rais wa Marekani, Donaled TrumpNA K-VIS BLOG NA Mashirika ya Habari
RAIS wa Marekani Donald Trump, amemfuta kazi Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey.
Bw.James Comey
Kwamujibu wa mashirika ya habari ya Kimataifa, Trump amemfukuza kazi bosi huyo wa shirika lenye “nguvu” kubwa ya upelelezi duniani, kwa kile kilichoelezwa jinsi alivyoshughulikia suala la barua pepe za mgombea kiti cha urasi wan chi hiyo mwaka 2016 Bibi Hillary Clinton.
Washington ilishtushwa na taarifa za Ikulu ya Marekani (White House), kuwa Comey ameondolewa kwenye wadhifa wake na kufutwa kazi.
Hata hivyo maafisa wa chama cha Democrats anachotokaBibiClinton wamesema kufutwa kazi kwa Comey kunatokana na FBIkuvujisha siri ya mahusianiano kati yakambi ya kampeni ya Trump na Mamlaka za Russia wakati wa uchaguzi mkuu wan chi hiyo uliomkutanisha Trump na Bibi Clinton.
Ikulu ya White Hosue imesema sasa anatafutwa wa kumrithi Comey mara moja.Reactions:

0 comments:

Post a Comment