Saturday, 13 May 2017


 Treni ya abiria iliyokuwa ikitokea jijini Dar es salaam kwenda Mikoa ya Tabora, Mwanza na Kigoma, imepata ajali usiku wa kuamkia leo Mei 13, 2017 katika eneo la stesheni ya Mazimbu Mkoani Morogoro.
Kwa mujimu wa Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzani, Bw.
Bw.Midladjy Maez
Midladjy Maez amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano usiku baada ya Mabehewa matatu kuacha njia na mengine manne kuegama na kusababisha abiria mmoja alietambulika kwa jina la Ashura Mrisho aliyekuwa akitokea Ngerengere kwenda Tabora kujeruhiwa na baada ya kuangukiwa na mizigo. 
Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro ili kufanyika utaratibu wa kuwapangia usafiri mbadala abiria wa treni hiyo. Taarifa zaidi zitafuata wakati Uongozi wa TRL, Wahandisi na Mafundi wa reli wakishughulikia ajali hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment