Tuesday, 9 May 2017

TEMB1
Tembo wanne, (pichani), leo Mei 9, 2017, wameonekana kwenye mazingira ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),  na kuleta tafrani kubwa miongoni mwa wanafunzi na jumuiya nzima ya chuo. Hata hivyo wataalamu wamesema, Tembo hao ambao hawakuleta madhara yoyote, "walikuwa safarini", kwani eneo walikokuwa wakipita ni nia yao ya asili au shoroba na Tembo husifika kwa kutunza kumbukumbu kama njia aliipita miaka 50 iliyopita anaweza kurudia palepale na inawezekana ndilo lililotokea leo hii. Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori  walifika kwenye eneo hilo na kuchukua tahadhari kwa kuwaadhibiti ili wasilete madhara kwa wananchi.
TEMB2TEMB3
Reactions:

0 comments:

Post a Comment