Friday, 12 May 2017ALIYEWAHI kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu amefariki dunia katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), ya Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam mapema leo Mei 12, 2017.
Taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema, Marehemu Mwambungu alikuwa akipatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo.
Kabla ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Marehemu Mwambungu alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkuu wa Wilaya ya Morogoro, na pia kwenyer Chama chaMapinduzi CCM. Munguailaze roho ya marehemumahala pema peponiAmin.
 

 Marehemu Mwambungu enzi za uhai wake, hapa akiongoza wananchi mkoani Ruvuma katikazoezi la kufanya usafi mapema mwaka jana.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment