Sunday, 14 May 2017

Mo Dewji


MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe na mwanachama tajiri wa klabu hiyo, Mohammed Dewj (Mo), waechukizwa na mkataba wa “kimya kimya” ambao Simba imeingia na SportPesa” hivi karibuni.
Tayari Hans Pope ameachia ngazi ya Uenyekiti wa kamati hiyo na hovyo kuzua sintofahamu ya Klabu hoyo ambayo inapigania kuwa bingwa wa soka Tanzania Bara ikichuana na hasimu wake mkuu Yanga pale kileleni.
Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi akiona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo
Zacharia Hans Pope
“Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo
"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili
"Kilichomchukiza, kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hana Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."

Na upande mwingine, uongozi wa Simba na umemeguka baada ya Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji wa usajiri, Zacharia Hans Poppe ameandika barua ya kujiuzulu, naye pia akilalamikia kutoshirikishwa katika mkataba wa SportPesa.
Hans Poppe aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Kamati za Usajili na mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Bunju Complex, amethabitisha kujiuzulu kwake, lakini hakutaka kuzama ndani zaidi juu ya sakata hilo.
Ijumaa SportPesa Tanzania ilitangza rasmi udhamini wake wa miaka mitano kwa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, wenye thamani ya Sh. Bilioni 4.96.
Mkurugezi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kwamba wameingia mkataba huko kwa dhumuni la kuendeleza soka nchini na kuisaidia klabu ya Simba kufikia malengo yake.
Akifafanua, Tarimba ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa mahasimu wa Simba, Yanga alisema kwamba, katika mkataba wao kwa mwaka wa kwanza wadhamini hao watatoa Sh. Milioni 888 na miaka itakayofuata wataongeza asilimia 5 na miaka miwili ya mwisho watatoa Sh. Bilioni 1 na kwamba fedha hizo zitatolewa kwa awamu nne kwa mwaka.
Tarimba alisema kwamba Simba watapaswa kuyathibitisha matumizi ya fedha hizo kwamba yalifanyika kwa maendeleo ya soka.
Alisema licha ya mkataba huo, pia kutakuwa na motisha klabu hiyo ikishinda mataji, mfano kwa ubingwa wa Ligi Kuu watapewa zawadi ya Sh. Milioni 100.
“Pia ikishinda michuano kama (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) Kombe la Kagame pia watapewa zawadi na wakifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika watapata zawadi ya Milioni. 250,”alisema Tarimba.

Evans Aveva, Rais wa Simba
Reactions:

0 comments:

Post a Comment