Tuesday, 23 May 2017


NA K-VIS BLOG/N Mashirika ya Habari
POLISI wa Uingereza wanasema, wanamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 23, kuhusiana na tukio la mlipuko wa bomu lililoua watu 23 pamoja na mlipuaji katika shambulio la “kigaidi” lililotekelezwa usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa burudani ambapo mwanamuziki wa Pop kutoka Marekani Arian Grande alikuwa akitumbuiza mjini Mancester nchini Uingereza.
“Kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali cha Islamic State (IS) kimetangaza kuhusika na shambulio hilo. “Tunaweza kuthibitisha kuwa tunamshikilia kijana wa miaka 23 kusini mwa Manchester” Polisi wa Manchester wamesema kwenye mtandao wa Twitter leo Jumanne Mei 23, 2017.
Bomu la kienyeji lililipuka Jumatatu usiku mwishoni mwa onesho la muziki wakati maelfu ya watu wengi wao vijana, walikuwa wakihudhuria burudani ya muziki kwenye ukumbi wa burudani wa Manchester Kaskazini mwa Uingereza, Polisi wamesema.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment