Sunday, 7 May 2017
NA K-VIS BLOG,DODOMA
WABUNGE wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mei 8, 2017 wamekubali kukatwa posho ya siku moja ili ipelekwe kwa wafiwa wa wanafunzi 33, walimu wawili na dereva wa shule ya msingi Lucky Vincent.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliwauliza wabunge kama wako tayari kutoa poshi zao baada ya kupokea ushauri kutoka pande mbili bungeni, (CCM) na Upinzani.
“Nimepata ushauri kutoka pande mbili na kama ushauri huu mkinikubalia, basi itakuwa vizuri, tumeambiwa tukatwe posho zetu za siku moja ili tupeleke kwa wafiwa moja kwa moja, wagawane sawa kwa sawa, wafiwa, je mnaafiki jambo hilo?” aliuliza Spika Ndugai na kujibiwa kwa kauli mloja ya ndio. Jumla ya watoto wa shule waliokuwa wakisoma darasa la saba shule ya msingi Lucky Vincent iliyoko Olasiti jijini Arusha, walifariki dunia, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo la mto Malera, kata ya Rothia, wilayani Karatu Mei 6, 2017.
Katika ajali hiyo pia walimu wawili na dereva wa basi hilo nao pia walipoteza maisha. Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, atawaongoza watanzania katika ibada ya kuaga miili ya marehemu hao kwenye uwanja wa kumbukumbu ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment