Thursday, 11 May 2017

MJUMBE Maalum wa mzozo wa Libya, Rais Mstaafu wa awamau ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Libya Mhe. Fayaz Serraj jijini Tripoli, nchini Libya Mei 10, 2017. Dkt.Kikwete anaendelea na usuluhishi wa kutafuta suluhu ya mzozo wa ,iutawala nchini humo ambapo pamekuwa na makundi kadhaa yanayopigana tangu kuuawa kwa rais wa nchi hiyo Kanali Muaamar Gadaf. Mjumbe huyo wa AU, alitarajiwa kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali katika mzozo huo.
Akiwa jijini Tripoli, Rais Mstaafu na ujumbe wake kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekutana na Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Libya Mhe. Fayez Serraj na Rais wa Baraza Kuu la Libya (High State Council) Mhe Abdulrahman Asswehly.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment