Friday, 5 May 2017MBUNGE Tarime(vijijini), Mhe. John Heche, amehamishiwa kwenye hospitali ya taifa Muhimbilikwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuugua ghafla mjini Dodoma.

Heche alipata tatizo la afya na kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma jana alfajiri. Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian.
Tulimpokea Mhe. Heche alfajiri ya jana na kumpatia huduma na kwakuwa matibabu yake yanaratibiwa na Kliniki ya Bunge,
hivyo tulimpokea na kumhudumia kwa muda kabla taratibu za kumsafirisha hazijakamilika, tulipoambiwa ndege ya kumsafirisha ipo tayari, aliondolewa kwetu na kusafirishwa kwa ajili ya matibabu,”alieleza daktari huyo.

Awali, mbunge huyo alipata tatizo la afya na kulazimika kuwa chini ya uangalizi wa kitabibu. Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akijibu maswali ya wananchi walihoji hali ya mbunge huyo, ambaye ilikuwa ikielezwa kuwa hospitalini.

Kabla ya muda huo kuwadia, ilielezwa kuwa Heche alipata maumivu ya tumbo kabla hajapelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema Taifa, Tumaini Makene jana  alithibitisha taarifa ya kuugua ghafla kwa Heche na kuletwa jijini Dar es Salaam katika hospitali hiyo.

“Ni kweli Heche aliugua ghafla akiwa Bungeni huko Dodoma, alisafirishwa kwa ndege jana asubuhi saa moja na kuletwa Muhimbili ambako anaendelea na matibabu,” alisema Makene.

Ofisa Habari wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha kupokelewa Heche jana saa nne asubuhi na kwamba anaendelea na vipimo kubaini nini tatizo lake.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment