Friday, 5 May 2017

A 1
 Katibu wa Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmshauri ya Manispaa ya Dodoma ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Godwin Kunambi (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Katibu mbele ya wajumbe wa Baraza hilo katika Mkutano wa kawaida wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2016/2017 jana katika ukumbi wa Manispaa. Kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Jumanne Ngede.

unnamed
Diwani wa Kata ya Mtumba Manispaa ya Dodoma Edward Maboje akichangia taarifa iliyowasilishwa na Katibu wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo Godwin Kunambi iliyojumuisha agizo la Rais Dokta John Magufuli kuhusu uongozi wa Mkoa na wadau wote kuchunguza na kuishauri Serikali endapo kuna haja ya kuendelea au kutoendelea kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao (CDA). Madiwani kwa ujumla wao wamependekeza Mamlaka hiyo ivunjwe.
A
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma katika Ukumbi wa Manispaa hiyo jana. 
NA RAMADHANIJUMAOFISI YA MKURUGEN
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wameeleza kufurahishwa  kwao na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuundwa kwa timu itakayokuwa na kujumu la kufanya utafiti na kuishauri  Serikali endapo kuna haja ya kuendelea kuwa na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu, (CDA).
Wakichangia taarifa ya Katibu wa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo, Bw. Godwin Kunambia mbaye pia ndiye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, takriban wajumbe wote wa Baraza hilo walidai kuwa sasa imefika wakati Mamlaka hiyo ivunjwe kwani imekuwa ikisababisha migogoro mingi ya ardhi badala ya kuupanga Mji huo kwani ndio jukumu lao la msingi.
Madiwani wote waliopata fursa ya kuchangia taarifa hiyo walieleza kuwa, wananchi wa Manispaa ya Dodoma wamechoshwa na uwepo wa Mamlaka ya CDA na kwamba imewanyanyasa kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwapora ardhi zao bila kuzingatia sheria na taratibu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment