Friday, 5 May 2017NA K-VIS BLOG
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Abdulrahman Kinana, yuko salama na anaendelea vizuri na mapumziko, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, amewaambia waandishi wa habari mkoani Arusha leo Mei 5, 2017.
Polepole ameyasema hayo wakati akikamilisha ziara yake ya kikazi mkoani humo. “Nimezungumza naye jana, na ameniambia anaendelea vizuri, yuko madhubuti kabisa kuliko jana..” alisema Polepole.
Polepole amefafanua kuwa, pamoja na ushiriki wake katika shughuli na mikutano mbalimbali ya chama ikiwemo ule mkutano mkuu maalum wa CCH uliofanyika mjini Dodoma, afya ya Katibu Mkuu Kinana haikuwa nzuri na hivyo iliamuliwa apelekwe nje ya nchi kwa matibabu.
“Na anaporejea mgonjwa anapotoka hospitali huwa hakimbilii kazini, shambani moja kwa moja inashauriwa kitaalamu achukue muda kupumzika ili kuimarisha afya yake, na jana tumeongea nae na anaendelea vizuri.” Alitoa hakikisho Polepole.
Kinana amekuwa haonekani hadharani kwa muda sasa, tangu kumalizika kwa mkutano mkuu maalum wa CCM mjini Dodoma kiasi cha miezi miwili iliyopita.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment