Wednesday, 24 May 2017
TAARIFA YA KAMATI MAALUM ILIYOUNDWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KUCHUNGUZA MCHANGA ULIO KATIKA MAKONTENA YENYE MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA) YALIYOPO KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI TANZANIA.
Utangulizi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliteua Kamati maalum ya wajumbe wanane kuchunguza aina na viwango vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi. Uteuzi huo ulifanyika tarehe 29/03/2017. Wajumbe wa Kamati hiyo wana taaluma katika fani za jiolojia, kemia, uhandisi kemikali na uhandisi uchenjuaji madini.
Chimbuko la kufanyika kwa uchunguzi huu ni kutokana na ukweli kuwa viwango vya madini yaliyopo kwenye makinikia havijulikani, na hata mikataba ya uchenjuaji makinikia haipo wazi. Hali hii inaleta hisia kuwa nchi inaibiwa na hainufaiki na uchimbaji wa madini.
Katika kutekeleza uchunguzi huu, Kamati iliongozwa na Hadidu za Rejea zilizoridhiwa na Serikali ambazo ni: 1. Kufanya uchunguzi kwenye Makinikia yaliyopo Bandari ya Dar es Salaam, Bandari Kavu na migodini kwa kupekua na kubaini vitu vilivyomo ndani pamoja na kuchukua sampuli za makinikia ili kuzifanyia uchunguzi wa kimaabara.
2 of 13
2. Kufanya uchunguzi wa kimaabara na kubainisha aina, kiasi na viwango vya madini yatakayoonekana katika makinikia kisha kubainisha thamani ya madini hayo.
3. Kutumia mitambo ya scanners iliyopo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kujiridhisha na aina ya shehena zilizomo kwenye makontena yenye mchanga wa madini; hii ni pamoja na kubainisha uwezo wa scanners hizo kuona vitu vyenye ukubwa na maumbile tofauti vilivyomo ndani ya makontena yenye makinikia.
4. Kuchunguza utendaji wa Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) wa kuchukua sampuli za makinikia, uchunguzi wa madini kwenye maabara na utaratibu wa ufungaji wa utepe wa udhibiti (seal) kwenye makontena kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
5. Kamati pale itakapoona inafaa inaweza kuongeza Hadidu za Rejea katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, Kamati itakuwa na mamlaka ya kumwita mtu yeyote kwa lengo la kupata taarifa.
Utekelezaji wa Majukumu
Ili kutekeleza uchunguzi huu, Kamati ilifanya yafuatayo: 1. Kuandaa mpango kazi. 2. Kukusanya nyaraka na taarifa mbalimbali kuhusiana na makontena yenye makinikia yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi. 3. Kutembelea maeneo yote yenye makontena yenye shehena za makinikia ili kuyachunguza na kuchukua sampuli zake. Maeneo hayo ni Bandari
3 of 13
ya Dar es Salaam, Bandari Kavu – ZAM CARGO na migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi. 4. Kutathmini uwezo wa scanners wa kuonesha makinikia yaliyomo ndani ya makontena pamoja na vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa ndani ya makinikia. 5. Kufanya uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za makinikia na kubaini aina, viwango na kiasi cha madini yaliyomo kwenye makinikia. 6. Kukokotoa thamani ya madini yaliyopimwa kwenye makinikia kwa kutumia viwango vilivyopatikana kutokana na uchunguzi wa kimaabara pamoja na thamani ya madini hayo kwenye soko la dunia. 7. Kuchunguza utendaji wa Wakala wa Serikali (TMAA) wa kukagua na kudhibiti uzalishaji na usafirishaji wa makinikia.
Matokeo ya Uchunguzi
Matokeo makuu ya uchunguzi huu ni yafuatayo:
1. Dhahabu Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720). Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).
4 of 13
Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.
Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000). Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.
2. Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%, wastani wa 27%).
Copper Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina
5 of 13
thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3.
Nyaraka za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa kiwango cha copper cha 20%. Kiwango hiki ni sawa na tani 4 za copper kwenye kila kontena; hivyo makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na tani 1,108 za copper. Kiasi hiki cha copper kina thamami ya USD 6,204,800 sawa na TZS bilioni 13.6. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa copper nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa ukizingatia kuwa usafirishaji wa makinikia nje ya nchi umefanyika kwa muda mrefu.
Silver Wastani wa kiwango cha silver kilichopimwa ni 6.1 kg na kiwango cha juu ni 7 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa silver kwenye makontena 277 ni 1,689 kg (tani 1.7) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.1 (USD 937,446); kiasi cha juu ni 1,939 kg (tani 1.9) ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.4 (USD 1,075,757). Hivyo, thamani ya silver katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.1 na bilioni 2.4.
Nyaraka za usafirishaji ambazo Kamati ilizipata kutoka bandarini zinaonesha kuwa makinikia yana silver kwa wastani wa takriban 150 g/t. Kiwango hiki kinamaanisha kuwa kuna 3 kg za silver kwenye kila kontena la tani 20 za makinikia. Kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, kiasi cha silver kilichopo kwenye nyaraka za usafirishaji ni 831 kg. Kiasi hiki cha silver kina thamami ya USD
6 of 13
461,039 sawa na TZS bilioni 1.0. Kwa takwimu hizi, kwa upande wa silver nako kuna upotevu mkubwa wa mapato ya taifa.

7 of 13
Sulfur Wastani wa sulfur uliopimwa ni tani 7.8 wakati kiwango cha juu kilikuwa tani 10.2, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa tani 2,161 za sulfur, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.4 (USD 648,130); na kiasi cha juu ni tani 2,825.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 1.9 (USD 844,296). Hivyo, thamani ya sulfur katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.4 na bilioni 4.9. Thamani hii ya sulfur ni kubwa ukizingatia kuwa haijawahi kutumika kukokotoa mrabaha katika mauzo ya makinikia.
Iron Wastani wa iron uliopimwa ni tani 5.4 wakati kiwango cha juu kilikuwa tani 6.1, kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa tani 1,496 za iron, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.3 (USD 1,047,060); na kiasi cha juu ni tani 1,695 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 2.6 (USD 1,186,668). Hivyo, thamani ya iron katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 2.3 na bilioni 2.6. Kama ilivyo kwa sulfur, thamani hii ya iron ni kubwa ukizingatia kuwa haijawahi kutumika kukokotoa mrabaha katika mauzo ya makinikia. Hali hii inazidi kuonesha jinsi gani nchi yetu isivyofaidika na uuzwaji wa makinikia nje ya nchi.
3. Uchunguzi pia umeonesha kuwepo kwa madini mkakati (strategic metals) ambayo kwa sasa hivi yanahitajika sana duniani na yana thamani kubwa sambamba na thamani ya dhahabu. Madini hayo ni: iridium, rhodium, ytterbium, beryllium, tantalum na lithium.
8 of 13
Iridium Wastani wa iridium uliopimwa ni 6.4 kg wakati kiwango cha juu ni 13.75 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, yatakuwa na wastani wa 1,773 kg za iridium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 108 (USD 48,876,096); wakati kiasi cha juu ni 3,808.8 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 231.0 (USD 105,007, 238). Hivyo, thamani ya iridium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 108 na bilioni 231.
Rhodium  Wastani wa rhodium uliopimwa ni 0.034 kg wakati kiwango cha juu ni 0.078 kg kwa kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 9.4 kg za rhodium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 0.7 (USD 300,731); wakati kiasi cha juu ni 21.6 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.5 (USD 689,912). Hivyo, thamani ya rhodium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 0.7 na bilioni 1.5.
Ytterbium Ytterbium ilipatikana kuwa na wastani wa 3.7 kg na kiwango cha juu kilikuwa 4.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 1024.9 kg za ytterbium, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 12.4 (USD 5,636,950); wakati kiasi cha juu ni 1,357.3 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 16.4 (USD 7,465,150). Hivyo, thamani ya ytterbium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 12.4 na bilioni 16.4.
9 of 13
Beryllium Wastani wa kiasi cha beryllium kilichopimwa ni 19.4 kg na kiasi cha juu kilikuwa 26.9 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, wastani wa beryllium kwenye makontena 277 ni tani 5.4 zenye thamani ya TZS bilioni 6.0 (USD 2,719,143); na kiwango cha juu kilichopimwa katika makontena 277 ni tani 7.5 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 8.3 (USD 3,770,358). Hivyo, thamani ya beryllium katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 6.0 na bilioni 8.3.
Tantalum Tantalum ilipatikana kuwa na wastani wa 11.7 kg na kiwango cha juu kilikuwa 17.3 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini yatakuwa na wastani wa 3240.9 kg za tantalum, ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.9 (USD 855,598); wakati kiasi cha juu ni 4,792 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 2.8 (USD 1,265,114). Hivyo, thamani ya tantalum katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.9 na bilioni 2.8.
Lithium Wastani wa kiasi cha lithium kilichopimwa ni 21.5 kg na kiasi cha juu kilikuwa 29.8 kg kwa kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, wastani wa lithium kwenye makontena 277 ni 5,955.5 kg zenye thamani ya TZS bilioni 1.0 (USD 468,698); na kiwango cha juu kilichopimwa katika makontena 277 ni 8,254.6 kg ambazo thamani yake ni TZS bilioni 1.4 (USD 649,637). Hivyo, thamani ya lithium
10 of 13
katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 1.0 na bilioni 1.4.
Jumla ya thamani ya aina zote za Metali Mkakati katika makontena 277 yaliyoko bandarini ni kati ya TZS bilioni 129.5 na bilioni 261.5. Pamoja na kuwa na thamani kubwa, metali hizi hazikuwa zinajulikana kuwemo kwenye makinikia na hivyo hazijawahi kujumuishwa kwenye kukokotoa mrabaha na hivyo kuikosesha Serikali mapato makubwa kwa kipindi chote cha biashara ya makinikia.
4. Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu.
5. Thamani zote za madini kwenye makinikia yaliyo ndani ya makontena zilizoainishwa hapo juu, zimepatikana kwa kutumia uzito wa wastani wa tani 20 za makinikia kwenye kila kontena. Hata hivyo, katika kupima uzito wa makinikia ndani ya makontena, kuna makontena kadhaa yaliyokuwa na uzito zaidi ya tani 20 za makinikia, kwa mfano makontena yenye namba CAIU 2461301, TCLU 0701267, MRKU 6880530 na MSKU 4280570 yalikuwa na makinikia yenye uzito wa tani 23.1; 22.9; 22.7 na 22.2, kwa mtiririko huo. Hivyo basi, ongezeko hili la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza upotevu zaidi wa mapato ya Serikali.
11 of 13
6. Pamoja na kuchunguza makinikia, Kamati pia ilichunguza shehena ya mbale za copper ndani ya makontena matano (5) yaliyozuiliwa bandarini. Sampuli za mbale hizo zilipatikana kuwa na viwango vya dhahabu hadi kufikia 38.3 g/t, viwango ambavyo havikuoneshwa kwenye ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA, na hivyo kutotumika katika kukokotoa malipo ya mrabaha Serikalini.
7. Uchunguzi wa Kamati kuhusu utendaji wa Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) umebaini kuwa Wakala haufungi utepe wa udhibiti mara baada ya kuchukua sampuli kwenye makontena. Ufungaji wa utepe wa udhibiti hufanyika baada ya siku kadhaa katika hatua za mwisho za usafirishaji wa makontena. Hali hii inatoa mianya ya kufanyika udanganyifu wa kiasi, viwango na thamani ya makinikia baada ya uchukuzi wa sampuli.
8. Kamati pia ilichunguza uwezo wa scanner inayotumika bandarini kukagua vilivyomo ndani ya makontena. Katika uchunguzi huu, ilibainika kuwa scanner hiyo haina uwezo wa kuonesha vitu vilivyomo ndani ya makinikia bali inaonesha umbo tu la shehena ya makinikia.
Mapendekezo
Kutokana na matokeo ya uchunguzi huu yanayoonesha upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi, ni muhimu Serikali kuchukua hatua zifuatazo haraka iwezekanavyo: 1. Serikali iendelee kusitisha usafirishaji mchanga wa madini “makinikia” nje ya nchi mpaka pale mrabaha stahiki utakapolipwa Serikalini kwa
12 of 13
kuzingatia thamani halisi ya makinikia kama ilivyoainishwa kwenye uchunguzi huu. 2. Serikali ihakikishe kuwa ujenzi wa smelters nchini unafanyika haraka ili makinikia yote yachenjuliwe nchini. Hii itawezesha madini yote yaliyomo kwenye makinikia kufahamika na kutozwa mrabaha halisi. 3. TMAA inatakiwa kufunga tepe za udhibiti kwenye makontena mara tu baada ya kuchukua sampuli ili kudhibiti udanganyifu unaoweza kutokea baada ya uchukuzi wa sampuli. 4. TMAA ipime metali zote ambazo zipo kwenye makinikia na kutumia metali zenye thamani katika kukokotoa kiwango halisi cha mrabaha. 5. Kutokana na uwepo wa madini mbalimbali yenye viwango tofauti kwenye mbale, TMAA ipime viwango vya dhahabu na metali nyingine muhimu katika mbale zote zinazosafirishwa nje ya nchi, bila kujali kilichooneshwa kwenye andiko la msafirishaji wa mbale husika. Aidha, Wizara ya Nishati na Madini ibainishe tabia za mbale (aina za madini na viwango vyake) zilizomo kwenye vyanzo mbalimbali nchini. 6. Serikali ijumuishe metali zote zenye thamani katika kukokotoa mrabaha wa makinikia na mbale za madini mbalimbali. 7. Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na Wizara Mama kutokana na kutosimamia vyema tathmini ya viwango halisi vya madini/metali mbalimbali vilivyopo katika makinikia na mbale za madini mengine; viwango ambavyo hutumika katika kukokotoa mrabaha. 8. Serikali ifanye uchunguzi wa kushtukiza kwa kadri itakavyowezekana katika udhibiti wa uzalishaji na usafirishaji wa madini nje ya nchi ili kujiridhisha kuwa taratibu zilizowekwa kisheria zinatumika ipasavyo. 9. Uchunguzi zaidi ufanywe na wataalam wa mionzi kwenye scanner zinazotumika bandarini ili kubaini aina au mfumo sahihi wa scanner unaofaa katika kuchunguza mizigo yenye tabia (properties) kama za makinikia na mbale za madini mbalimbali.
13 of 13
SHUKRANI
Kwanza kabisa, Kamati kwa heshma kubwa inapenda kutoa shukrani kwako wewe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuwa na imani nasi na kututeua kutekeleza jukumu hili muhimu la kuchunguza aina na viwango mbalimbali vya madini katika makinikia ili kuweza kuondokana na upotevu mkubwa wa pato la taifa kupitia biashara ya makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi. Ni matumaini yetu kuwa matokeo ya uchunguzi huu yatasaidia Serikali kupitia sekta ya madini katika kuchangia pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi yetu.
Kamati pia inatoa shukrani za dhati kwa Katibu Mkuu Kiongozi na wasaidizi wake wote kwa misaada na ushirikiano wao uliowezesha Kamati kutekeleza majukumu yake vizuri.
Aidha, Kamati inatambua na kuthamini michango iliyotolewa na taasisi mbalimbali zikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini, Wakala wa Jiolojia Tanzania, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Bandari Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro.

14 of 13
Mheshimiwa Rais, kwa heshma kubwa sasa nachukua fursa hii kwa niaba ya Kamati, kukukabidhi nakala sita za Ripoti kamili ya uchunguzi huu. Ninakuomba uzipokee.
Pia ninaomba nikukabidhi kifurushi chenye nyaraka zote ambazo Kamati ilizikusanya kutoka kwenye taasisi za Serikali zinazohusika katika kusimamia na kudhibiti usafirishaji wa makinika nje ya nchi, pamoja na nyaraka kutoka kwa wadau mbalimbali wanaohusika katika biashara ya makinikia.
Aidha, nichukue fursa hii kukufahamisha kwamba sampuli zote za makinikia na mbale za copper zilizochukuliwa na Kamati na kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara, zimehifadhiwa ndani ya kontena moja ambalo liko mahali salama chini ya uangalizi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali. Kwa heshma kubwa ninaomba nikukabidhi funguo za kontena lililohifadhi sampuli hizo.
Ninaomba kuwasilisha

Brad Gordon, Aifa Mtendaji Mkuu wa ACACIA

Reactions:

0 comments:

Post a Comment