Monday, 15 May 2017NA K-VS BLOG
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, “amebadili gia angani” mapema leo Mei 15, 2017 baada ya kufuta uamuzi wake wa jana wa kujiuzulu wadhifa huo na kutangaza kuwa amebadili maamuzi yake.

Uamuzi wa Hans Poppe kurejea kwenye nafasi yake umekuja siku moja tu, baada ya kiongozi huyo kutangaza kujiondoa kwenye nafasi hiyo kwa kile alichodai kuchukizwa na taratibu zilizotumika kuiingiza Klabu ya Simba kwenye mkataba wa miaka minne na kampuni ya Sportpesa ya Uingereza.

Hans Poppe amethibitisha kurejea kwake kundini baada ya mkutano na viongozi wa Simba.
 “Kweli tumekutana usiku kucha hadi saa 9 ya kuamkia leo Mei 15, 2017, na tumekubaliana na tumeyamaliza vizuri. Huu ni wakati wa kusonga mbele,” alisema Hans Poppe.
Hata hivyo mfanyabiashara maarufu na mfadhili wa Simba, Mohammed Dewji ambaye naye alichukizwa na uamuzi wa viongozi wa Simba kuingia mkataba na kampuni hiyo bila hata kumjulisha yeye aliutaka uongozi wa klabu hiyo kumlipa fedha zake zaidi ya shilinginbilioni 1 ambazo amekuwa akilipa wachezaji na benchi la ufundi la Simba kama mishahara kwa makubaliano kuwa watamlipa fedha hizo pindi uamuzi wa Dewji kununua hisa za Simba utakapopitishwa.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment