Wednesday, 10 May 2017KAMATI Kuu ya Act Wazalendo imemuidhinisha Ndugu Dorothy Jonas Semu(pichani), kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Dorothy Semu amewahi kushika nafasi za ukatibu wa Kamati za Sera, Mipango na Utafiti na Kamati ya Fedha na Miradi.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe, kupitiaukurasa wake wa Facebook amesema, Ndugu Dorothy Semu ametoa mchango mkubwa kwa chama hasa kwenye uandaaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 na masuala mengi ya kiutafiti juu ya sera na mikakati ya Chama.
Ndugu Semu ni mtaalamu wa masuala ya Fiziotherapia mwenye shahada mbili za eneo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika ya Kusini. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 wa kufanya kazi kwenye nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Asasi za kiraia ikiwemo Mratibu wa kuzuia ulemavu kwenye Programu ya Taifa ya Kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma.
Tunamtakia kila la heri Ndugu Dorothy Semu kwenye utekelezaji wa majukumu yake.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment