Tuesday, 16 May 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Nd,Abdalla Ali Mohamed Mwananchi wa Makondeko Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakati alipofika Nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa Wananchi waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,Rais alifika katika shehia hiyo leo Mei 16, 2017 wakati alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  Wananchi, na  kutoa mkono wa pole,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.(PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR)

Wataoto wa maeneo ya Nyarugusu Wilaya ya Mjini,Unguja wakimuangalia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe kuwafariji na kutoa pole kwa wananchi walioathirika na Nyumba zao zilizobomoka kutokana na Upepo mkali uliotokea jana katika maeneo yao na kupelekea uharibifu kwa kung'oka mapaa ya Nyumba wanazoishi, wakati alipofanya ziara maalum leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe leo alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  wananchi ambao Nyumba zao zimepata athari ya kun'goka kwa mapaa   kutokana na Upepo mkali uliosabisha   na  uharibifu   huo jana, ambao  umepelekea kukosa pahala pa kuishi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza Waandishi wa Habari baada ya kuwafariji na kutoa pole kwa Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kung'oka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,  wakati alipofanya ziara maalum  leo akiwa na Viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo
Reactions:

0 comments:

Post a Comment