Friday, 26 May 2017

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ,
Dk. Juliana Palangyo amewaagiza wahandisi wa Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara nchini Tanroads kufanya nguvu kwa pamoja ili kuweka alama za miundombinu ya mradi wa kuboresha umeme jijini Dar es Salaam. 
Dk .Palangyo amesema hayo jijini Dar es Salaam leo Mei 26, 2017 alipokuwa akikagua sehemu ya miundombinu hiyo itakayopita barabara ya Mandela kuelekea kituo cha umeme cha Kurasini wilayani Temeke.
“Tanesco wamekubaliana na Wakala wa Barabara nchini kupitisha sehemu ya miundombinu ya umeme kando kando mwa barabra ya Mandela hili kuweza kuongeza nguvu katika kituo cha kurasini na mkoa mzima wa Dar es Salaam.Makabuliano haya yamefikiwa leo mara baada ya mimi kutembelea katika ofsi za Tanroads na sehemu ambapo miundombinu hiyo itatakiwa kupita”.
Dkt. Palangyo amesema kuwa wameamua kufanya mazungumzo na Tanroads hili kufikia muafaka kwakuwa wao nao walitaka kutumia eneo hilo katika moja ya miradi yao hivyo kufikia muafaka wa hili kumewezesha mradi wa tanesco kwenda kwa kasi zaidi ya awali.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment