Monday, 22 May 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisikiliza malalamiko ya wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam wakielezea adha wanayokumbana nayo kutokana na uharibifu wa Daraja
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori  sambamba na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally wakikagua daraja lililovunjika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Muonekano wa Daraja la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam likiwa limeharibika
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam

  Mwananchi akizungumza
Na Nasri Bakari, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo Jumamosi, Mei 20, 2017 ameagiza kujengwa kwa daraja  jipya kutokana na kuharibika kwa daraja la awali katika eneo la Msumi Kata ya Mbezi Jijini Dar es salaam.
Agizo hilo amelitoa mapema hii leo wakati akizungumza Na wananchi waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara uliowajumuisha pia Mtendaji wa Kata,  wajumbe wa mitaa na wataalamu mbalimbali kutoka Manispaa ya Ubungo.
Mhe Makori amesema kuwa amejionea adha  iliyopo katika daraja hilo ambapo sio ubovu wa miundombinu pekee bali pia ni swala la usalama hasa kwa watoto wanaopita katika daraja hilo waendapo shuleni na sehemu mbalimbali.
"Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hii sitojisikia vizuri kuona tunahatarisha maisha ya binadamu kwa namna yoyote ile, lazima nihakikishe mnakuwa salama wakati wote"
"Hivyo nakuagiza Mkurugenzi kuanza haraka ujenzi wa daraja hili ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidi wananchi Wetu hawa  kupita kwa usalama zaidi" Alisema Mhe Makori.
Aidha amesisitiza kuwa kodi zinazokusanywa na serikali  ni kwa ajili ya kugharamia na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kama vile kuboresha Sekta ya Elimu, Afya na huduma nyingine za kijamii, hivyo ni lazima  serikali ishughulikie na kusimamia mahitaji ya Msingi kwa wananchi wake.
Sambamba na hayo pia Mhe Makori amewaomba wananchi kufika kwa viongozi wao pindi wanapopata kadhia mbalimbali zinazowasumbua katika jamii inayowazunguka kwani wameajiriwa kwa ajili yao na serikali ya awamu ya tano inajali wananchi wote hususani wanyonge.
Kwa upande wake Injinia wa Ujenzi Manispaa ya Ubungo Ndg Goodluck Mbanga amesema kuwa daraja lililokuwa limejengwa awali lilikuwa Dogo ukilinganisha Na wingi wa Maji Jambo lililopelekea kuharibika haraka.
Mbanga Alisema utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya nitaanza haraka iwezekanavyo ili kufikia mwanzoni mwa mwaka 2018 lianze kutumiwa Na wananchi hao ambao wamepata adha kubwa kwa muda mrefu.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Msumi Ndg Hemed Abdallah Gulamu amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa Kazi kubwa anayoifanya tangu alipoteuliwa kuongoza Wilaya hiyo.
Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa ufanisi katika utendaji Na kusema kuwa uongozi wake utaacha alama kubwa na kukumbukwa na watanzania wote.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza katika Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kufika Shule ya Msingi Ubungo Plaza kwa ajili ya Mkutano uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua Mipaka ya eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkutano  uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally akijibu baadhi ya maswali ya wananchi wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo Na Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri wakisikiliza Maelezo kuhusu Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkuu wa Wilaya kuzuru shuleni hapo kwa ajili ya Mkutano
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi.

Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 19, 2017 ameagiza kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi  ambao waliohudhuriwa katika viwanja vya  shule ya Msingi Ubungo Plaza.
Mhe Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.
Alisema kuwa Kodi zinazokusanywa Na serikali kwa wananchi ni kwa ajili ya kuwaimarishia miundombinu kuboresha afya, na Elimu hivyo serikali ni lazima ishughulikie na Kusimamia shughuli zote ikiwemo Ujenzi wa madarasa kwa manufaa ya wanafunzi Na wananchi kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo hayo Wakati akijibu Risala iliyosomwa Na Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza Bi Theresa Masaba ambayo ilibainisha changamoto nyingi ikiwemo Ukosefu wa Vyoo Bora, Ukosefu wa Uzio, Uchakavu wa Majengo ya shule, Upungufu wa Majengo (Ofisi ya Walimu, Darasa la awali Jiko, Maktaba), Maji taka kuelekezwa kwenye eneo la shule, Eneo la shule kufanyika kama sehemu ya kuvutia bangi Wakati wa jioni na siku za Wikendi sambamba na Upungufu wa samani za shule.
Mhe Mkuu wa wilaya ameagiza pia kuvunjwa kwa Vyoo vilivyopo Na kujengwa Vyoo vingine vipya sambamba na kujengwa kwa  uzio wa shule ili kuepuka kadhia ya watu wanaotumia kama Eneo la kuvutia bangi Na vitendo vingine viovu visivyo kubalika katika jamii.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha anawakamata watu wote wanajihusisha Na uvutaji bangi katika Eneo la shule kwani Jambo hilo halikubaliki si tu Na shule hiyo Bali Na serikali kwa ujumla.
Sambamba Na hayo pia Mkuu wa wilaya ameagiza kuvunjwa kwa ukuta wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) ambapo Uzio wake umejengwa ndani ya Eneo la shule.
Alisema kuwa Kanisa hilo tayari lilishapewa Notisi ya siku Saba tangu Mei 8 mwaka huu kwa ajili ya kuvunja ukuta huo lakini hawakufanya hivyo.
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Walimu Na wanafunzi wa shule, Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza Ndg Ramadhani Maughuu amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutembelea shule hiyo Na kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinaikabili shule hiyo kwa muda mrefu.
Maughuu ametoa pongezo zake pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwa ufanisi Na uchapa Kazi wake sambamba Na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa weledi Na ufanisi wa kuwahudumia watanzania Na kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment