Friday, 26 May 2017

 Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma leo Mei 26, 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho inayopatikana hapo chini, chama hicho kimeanza vikao nyeti vya chama mjini humo leo Ijumaa na kesho Jumamosi, Baraza Kuu la chama hicho litakutana mjini humo Jumamosi Mei 27. Katuka hatua nyingine, Msemaji wa chama hicho Tumaini Makene amekanusha vikali taarifa zinazodai kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt.Vincent Mashinji amejiuzulu wadhifa wake. Makene katika taarifa yake aliyoitoa mjini Dodoma amesema."Tumeona tweetter moja inayotembea tena ya kiongozi mmoja wa CCM na nimejibu nimesema kwamba taarifa hizi zinasambazwa na viongozi wa CCM, Katibu Mkuu yupo mjini Dodoma tangu Jumanne kwa sababu kuna kikao cha summit ya TDC, na jana alikuwa anaongoza kikao cha Sekretariati ya chama kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho na leo yuko kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama ambayo inaandaa agenda za kikao cha baraza kuu na Katibu Mkuu alikuwepo." Alisema Makene.Reactions:

0 comments:

Post a Comment