Sunday, 14 May 201711
Na Mahmoud Ahmad Kondoa
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kondoa limepitisha sheria ndogo ndogo zitakazo ongoza halmashauri hiyo sanjari na kupitisha miradi mbali mbali ya maendeleo iliyopangwa kwa robo ya tatu ya mwaka 2017\18 pamoja na miradi ya matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo.
Akisoma taarifa mbele ya baraza hilo mkurugenzi wa halmashauri hiyo Khalifa Kondo amesema halmashauri imeandaa mipango ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2017\18 kwenye sekta za barabara,Maji,Afya na miundombinu itakayosaidia kuboresha huduma kwa wananchi.
Amesema kuwa kwenye mradi wa kuboresha huduma ya maji halmashauri imeanda upanuzi wa huduma hiyo kwa kuongeza visima 9 ambavyo vitano vitakuwa kwenye maeneo ya mji huo na vine kwenye maeneo ya pembezoni vyenye thamani ya tsh.360 milion ambapo kwa sasa mpembuzi yakinifua anaendelea na kazi yake.
Kuhusu huduma za barabara wataendelea kuboresha kwa kutumia mapato ya ndani yanayotokana na makusanya ya halmashauri ilikuziweka katika hali nzuri kwa kupitisha greda kwenye maeneo ambayo yameharibiwa na mvua zinazoendelea kwa sasa kote nchini.
“Nimefurahishwa na uendeshaji wa vikao vya baraza kwani yale yote tuliowasilisha katika baraza letu yamejadiliwa kwa kina na kutishwa zikiwemo sheria za uendeshaji wa halmashauri yetu” aliongeza Kondo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Hamza Mafita  amesema kuwa baraza lake linaendeshwa kwa viwango katika kuhakikisha wananchi waliowachaguwa wanapata huduma za maendeleo kwa wakati ikiwemo huduma muhimu kwa jamii.
Amesisitiza kuwa wataendelea kuhakikisha halmashauri yao inakuwa ya mfano katika kuwahudumia wananchi sanjari na kuboresha huduma za kijamii na miradi ya maendelea inakamilika kwa wakati ilikuweza kutekeleza iliani ya uchaguzi ya ccm kwa kuisimamia halmashauri kutekeleza majukumu iliyojiwekea.
Nae Mbunge wa JImbo hilo Sanda alisema kuwa sula la mradi wa maji ndio wanalifuatilia katika wizara kuhakikisha fedha walizoomba zinatoka kwa wakati ilikutekeleza maradi taraji wa kuongeza kiwango katika huduma hiyo ilikuboresha na wananchi wa furahie uwepo wa serikali yao.
Sanda Amesema kuwa serikali imekuwa ikipanga bajeti ila fedha zinazotolewa zimekuwa hazifiki kwa wakati na hivyo akaiomba serikali kuhakikisha fedha zinazotengwa zinafika kwa wakati majimboni ilikuweza kukamilisha miradi iliyopangwa

Reactions:

0 comments:

Post a Comment