Tuesday, 18 April 2017


WANAJESHI
JESHI la Korea Kaskazini lina jumla ya wapiganaji 700,000 na wapiganaji wa akiba Milioni 4.5, kwa maneno mengine, robo ya raia wa Korea Kaskazini, wanaweza kuingia vitani wakati wowote watakapohitajika, ni kama vile hapa nchini, kuna mgambo lakini pia kuna wale wanaoingia kwenye mafunzo ya Kijeshi ya JTK, hawa unawea kuwalinganisha na jeshi la akiba.
Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanasema, kila Mwanamume nchini humo anatakiwa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi na anaweza kuhitajika kupigana wakati wowote panapolazimu na inasemekana jeshi la Korea Kaskazini linazidi lile la majirani zake. Korea Kusini kwa mara mbili.
SILAHA ZA KINYUKLIA
Licha ya malalamiko kutoka Jumuiya ya Kimataifa, Serikali ya Pyongyang haijafanya kificho kuhusu uwezo wake wa kinyuklia, smbamba na majaribio ya makombora ya masafa marefu, Korea Kaskazini imefanya majaribio ya silaha za kinyuklia mara tano, mawili ilifanya mwaka 2016 na kwamba moja kati ya hayo majaribio, kombora moja lilivishwa kichwa cha roketi.
UWEZO WA KIJESHI
Taarifa ya ya uwezo wa kijeshi wa majeshi Duniani ya mwaka 2016, ilionyesha Pyongyang ni moja kati ya mataifa yaliyofika mbali zaidi katika umiliki wa silaha. Ina nyambizi (Submarines), 70, vifaru 4,200, ndege za kivita 458, na ndege nyingine za kushambulia 572.
MAONYESHO MAKUBWA YA NGUVU ZA KIJESHI
Kila mwaka Pyongyang hufanya maonyesho ya kijeshi, mamia kwa maelfu ya wanajeshi na wananchi hujazana kwenye mitaa ya Pyongyang ili kushiriki kwenye paredi ya kijeshi. Na maandalizi ya maonyesho na mikutano hiyo hufanyika mwezi mmoja kabla na hufanywa wakati wa maadhimisho ya chama kinachotawala au familia ya Kim Jong Un.
MAREKANI YAPOTEZA UVUMILIVU
MWANZONI mwa mwezi huu wa Aprili, Marekani ilipeleka manowari ya kubeba ndege ijulikanayo kama Carl Vinson kwenye eneo la Rasi ya Korea, (Korean Peninsula), ikisema ilikuwa inachukua tahadhari dhidi ya vitendo vya Korea Kaskazini. Hatua hiyo ya Marekani iliamsha hasira lutoka Pyongrang na ikaonya itajibu mapigo kwa aina yoyote ile ya vita. Taarifa za kijasusi zinkadiria kuwa msuguano huu baina ya Marekani na Korea Kaskazini, hautachukua muda mrefu kabla ya luzua vita. Inaonyesha Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump anaweza kuamuru hali hiyo kutokea.
KAULI YA MIKE PENCE
Tayari Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence ametembelea eneo la Korea Kusini kiasi cha futi 100 kutoka eneo ambalo tayari majeshi ya Pyongyang yamejiweka tayari na ameiambia CNN kuwa Pyongyang lazima ielewe kuwa mikakati ya utawala wa Trump juu ya utawala wa Pyongyang uko tofauti sana na ule wa marais wa Marekani waliotangulia.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim akwia na maafisa wa juu wa kijeshi


Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence, akiwa kwenye eneo la DMZ huko Seoul Korea Kusini Aprili 17, 2017
Reactions:

0 comments:

Post a Comment