Wednesday, 19 April 2017NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MFUKO wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotewa na Mfuko huo
Maonnesho hayo yalifunguliwa rasmi Aprili 18, 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janeth Ezekiel, Mfuko huo unatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya utajikita zaidi katika kutoaa elimu juu ya mfumo wa ' Wote scheme' unaowezesha watu kutoka sekta isiyo rasmi kuwa wanachama.
“Wote Scheme unawahusu wale wote wanaojiajiri kama vile mama lishe, madereva wa boda boda, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, wasanii, wote hawa  wanaweza kujiunga na mpango huo ambapo pamoja na mambo mengine watafaidika kwa kuwa na fursa za huduma  za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao ya uzeeni.” Alisema Bi. Janeth
Kupitia Maonesho haya PPF inasajili wanachama  wapya hapo hapo viwanjani pamoja  na kukabidhi vitambulisho vya  uanachama wa “Wote Scheme”
Hivyo ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Mashujaa kupata elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu, alsiema. Aidha alisema  kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu  nao.Katika maonesho hayo yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alimkabidhi cheti cha udhamini, Meneja wa PPF Kanda  ya Mashariki na Kati, Bw.Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio.

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janeth Ezekiel, (kushoto), akitoa maelezo ya shughuli mbali mbali zitolewazo na PPF kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo wakati wa Maonesho hayo yanayoedelea kwenye viwanja vya Mashujaa mkoani Dodoma leo Aprili 19, 2017

Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matilo fursa apatazo mwanachama aliyejiunga na PPF kupitia Mfumo wa “Wote Scheme”

 Wananchi wa kada mbalimbali wakitembelea banda la PPF kwenye maonesho hayo

Meneja wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian, (kushoto), akimuelezea kazi za PPF  mmoja wa watu waliotembelea Maonesho hayo

 Maafisa wa PPF wakiwasikiliza kwa makini wananchi waliotembelea banda hilo
Picha ya pamoja
Reactions:

0 comments:

Post a Comment