Tuesday, 4 April 2017NA K-VS BLOG
WAVUVI 9 wanahofiwa kufa maji, baada ya boti yao kuzama jirani na kisiwa cha Tumbatu, kati ya Pemba na Zanzibar Alfajiri ya Aprili 4, 2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Zanzibar, Bw. Makarani Ahmed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine 44 wameokolewa.
Alisema, chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliotokea wakati wavuvi hao wakiwa majini na kwamba boti hiyo ilizama kufuatia mawimbo makubwa.
Bw. Ahmed alisema, boti hiyo inakadiriwa kuwa na wavuvi wapatao 52 na kwamba juhudi za kuwatafuta wavuvi wengine zinaendelea.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini, (TMA), ilitoa taarifa ya kutahadharisha uwepo wa mvua na upepo kuanzai jana Aprili 4.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment