Tuesday, 4 April 2017WATANZANIA wanane wametiwa hatiani na mahakama moja nchini Malawi, kufuatia kesi ya kijasusi iliyokuwa ikiwakabili.
Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kaskazini, Texious Masoamphambe, amesema, kuingia kwenye eneo la mgodi wa Urani wa Kayelekera bila kutoa taarifa, Watanzania hawa wametenda kosa la jinai la kuingia eneo bila ruhusa, (trespassing”, kufanya shugjuli za uchunguzi bila ruhusa au leseni ambapo ni kinyume na kifungu cha 314 (1) cha sheria na kifungu 2 cha sheria za uchimbaji na madini
Wawili kati yao walikiri kutenda kosa hilo huku wengine sita wakikanusha katu katu makosa yote na kusisitiza kuwa walifika pale kwa ziara ya kimafunzo, (Study tour) kwa msada wa raia wa Malawi.
Bob Mtekama, ni afisa mwandamizi wa upelelezi wa polisia nchini Malawi na katika hati ya mashtaka alisema polisi ilipewa taarifa kwamba Watanzania hao walipanga kutembelea eneo hilo la Kayelekera na polisi ikaweka mtego na kuwakamata Watanzania hao.
“Walikutwa na camera, kompyuta, ramani ya mgodi na vifaa vingine.” Alisema afisa huyo wa upelelezi.
Alisema watuhumiwa hawakuwa na vibali kutoka serikalini kutembelea mgodi huo uliofungwa na hivyo ilitia shaka.
Kesi ya Watanzania hao wanane kutoka taasisi ya kibinafsi ya Kanisa Katoliki huko Songea, (TUAM) ilianza kusikilizwa Januari 17, 2017.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment