Wednesday, 26 April 2017


NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI
WANANDOA waliodumu katika ndoa kwa miaka 69, wamefariki dunia kwa kupishana saa moja.
Familia ya wanandoa hao waliokuwa wakiishi Illinois nchini Marekani, wameliambia Shirika la Habari la Uingereza BBC, kuwa Isack Vatkin (91), alikuwa amekamata mikono ya mkewe Teresa (89), pale alipopatwa na maradhi ya Alzheimer yaliyopelekea kifo, Jumamosi iliyoipia, gazeti la Daily Herald la Illinois liliripoti.
Bw.Isaac(mume), naye alifariki dakika 40 baadaye, familia yake ilisema na kuongeza, “huwezi kupenda kuona wanaondoka” alisema mjukuu William Vatkin, unaweza kuomba kwa jambo linguine lolote, alisema.
“Mapenzi yao yalikuwa madhubuti, kwa kifupi hawakuweza kuishi tofauti” alisema binti ya marehemu wanandoa hao, Clara Gesklin wakati wa mazishi yao ya pamoja. “siku zote walikuwa katika upendo hadi umauti katika sekunde ya mwisho” alisema Rabbi Barry Schechter, ambaye ndiye akiyeongoza ibada ya mazishi nyumbani nje kidogo ya Chicago kwenye mji wa Arlington Heights.
Wafanyakazi wa hospitali ya Park waliwakuta Bwana na Bibi Vatkin, wakiwa hawajibu kitu na walikuwa wakipumua kwa shida sana Jumamosi na wakaamua kuwalaza vitanda jirani na wanafamilia, waliwashikanisha mikono yao.
Marehemu hao wameacha watatu huko Skokie, Illinois na walikuwa na ukaribu mkubwa na wajukuu zao, familia ilisema.
Bw. Vatkin alikuwa msambaza nyama maarufu na Bibi Vatkin yeye alikuwa mama wa nyumbaniReactions:

0 comments:

Post a Comment