Saturday, 1 April 2017NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
UWEKEZAJI mkubwa unaofanywa na Mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Said Salim Bakhresa, utabadilisha kabisa muonekano wa Kisiwa cha Unguja huko Zanzibar na hivyo kuwa moja ya visiwa vyenye kuvutia zaidi kwenye ukanda huu wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi.
Kisiwa cha Unguja ambacho ni moja ya visiwa viwili kikiwemo cha Pemba, vinavyoifanya Zanzibar, kwa sasa uchumi wake unategemea zaidi utalii.
Bw. Bakhresa kwa kuona fursa hiyo, ameamua kuwekeza katika miundombinu rafiki kwa ajili ya shughuli za utalii ambapo kwa sasa miradi mikubwa miwili ya uwekezaji wa miundombinu hiyo tayari inaendelea na inakaribia kufikia ukingoni.
Machi 31, 2017, Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, waliokuwa kisiwani humo kuhudhuria semina ya mafunzo ya wiki moja iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), walipatabfursa ya kutembelea miradi hiyo ya Bw. Bakhresa.
Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ndiye msemaji mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, waandishi hao wamejionea uwekezaji huo mkubwa unaofanywa na Mfanyabiashara huyo.
Waandishi hao walitembelea miradi mitatu mikubwa ya kiuchumi, ikiwemo ule wa ujenzi wa Hoteli kubwa ya kitalii na eneo la kupumzikia na michezo ya aina mbalimbali ya nchi kavu na baharini, eneo la Mtoni, mradi huu unajulikana kama mradi wa (Mtoni- Marine), pia walitembelea mradi mwingine mkubwa wa ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi eneo la Fumba kilomita chache kutoka eneo la katikati ya mji wa Unguja, (Stone Town), na mradi mwingine ambao tayari umeshaanza  kufanya kazi ni kiwanda kikubwa cha maziwa hapo hapo Fumba.
Akizunhumzia mradi wa Mtoni Marine, Meneja mradi Bw.Karama Awadh, alisema, “Mradi Umegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa vyumba vya kulala wageni, (Hoteli), huku sehemu ya pili ni uhamishaji maji ya bahari, (Land reclamation)”.Alisema.
Akifafanua zaidi, Bw. Awadh alisema, upande wa mradi wa vyumba, jumla ya vyumba 106 vimejenwga huku 6 kati ya hivyo vina hadhi ya makazi ya Rais, (Presidential suit).
Kwa upande wa sehemu ya pili ya uhamishaji maji eneo lenye urefu wa mita 450 na upana wa mita 250. litahusika.” Eneo hilo lililojazwa mchanga ni kwa ajili ya watu kupumzika, patakiuwepo na michezo ya maji, (water-park), watu wa kila aina wakiwa na familia zao wapatao 3,500 watahudumiwa kila siku kwa wakayi mmoja sehemu ya Marina itakuwa na huduma za kuegesha boti 30 zenye urefu wa mita 10”. Alisema.
Aidha mradi mwingine mkubwa ni ule wa Fumba uptown Living, Zanzibar, ambapo nyumba za kisasa 500 zinajengwa kandokando ya bahari. 
Nyumba hizo hatimaye zitauzwa kwa watu watakao hitaji, wageni na wenyeji.

 Meneja Mradi wa Mtoni Marine ulioko kisiwani Unhuja, Zanzibar, Bw.Bw.Karama Awadh,(wapili kushoto), akiwaongoza maafisa wa BoT, na waandishi wa habari za uchumi wakiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (wakwanza kulia), walipotembelea mradi wa Mtoni Marine, Machi 31, 2017.
 Maafisa wa BoT, waandishi wakiongozwa na Bw. Awadh kutembelea mradi huo
Mashine ya kufyonza maji ikiwa kazini katika zoezi la Land reclamation
 Kifyonza maji namchanga baharini kikiwa kazini
 Hili ni moja ya mabomba makubwa yanayopitisha maji na mchanga uliofyonzwa baharini na kuhamishia nchi kavu
 Meneja mradi Bw.Karama Awadh, akizungumza na waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, baada ya kutembelea mradi huo
 Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina, (kushoto), Afisa Uhusianio Mkuu wa idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bw. Lwaga Mwambande, na Aisa katika ofisi ya Uhusiano na Itifaki, Bi. Flora
 Dkt. Hassan Abbasi, (kulia), akimuelekeza Bi. Vicky Msina, kusafisha viatu kabla ya kuruhusiwa kuingia ndani ya kiwanda cha Maziwa cha Bakhresa kilichoko Fumba
 Usafi unazingatiwa vilivyo kabla ya kuingia ndani ya kiwanda
 Vifungashio vya Maziwa
 Vinu vya kuchanganya unga wa maziwa, maji na virutubisho vingine
 Maziwa yakiwekwa ndani ya maboksi na wafanyakazi mahiri
 Mfanyakazi mwenye uso wa furaha, akisimamia jinsi maziwa yanavyosafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutumia mitambo inayoendeshwa kwa kompyuta
 Mifuko ya Maziwa ya Unga
 Mradi wa ujenzi wa nyumba wa Fumba Uptown Living, Zanzibar

 Afisa wa kiwanda cha maziwa, akiwaleza waandishi wa habari shughuli za uzalishaji maziwa kiwandani hapoReactions:

0 comments:

Post a Comment