Monday, 3 April 2017Binti  aliyetambuliwa kwa jina la Hudhaima  mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Kikwajuni, amejitosa baharini leo Aprili 3, 2017 akiwa kwenye boti ya Kilimanjaro 5.
Taarifa zinasema binti huyo alitoroka kwao na kwenda Dar es Salaam, akimfuata “mpenzi” wake kitendo kilichomlazimu  mjomba wake kumfuata Dar es Salaam na kumrejesha Zanzibar na walipokuwa safarini kwenye boti hiyo wakikaribia bandari kuu ya Zanzibar, kwenye kisiwa cha Chumbe, ndipo binti huyo alijitosa baharini kwa nia ya kujiua. Taarifa zinasema, baada ya mjomba kuona kitendo hicho alipiga kelele za kuomba msaada na ndipo
mabaharia (wapiga mbizi) wa boti hiyo, haraka haraka walijitosa baharini na kumuokoa binti huyo ambaye tayari alikuwa hoi bin taaban. Taarifa zaidi zinasema, binti huyo anaendelea vizuri.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment